MWONGOZO WA KISASA WA UFUGAJI WA KUKU
UTANGULIZI Kuku ni mifugo kama ilivyo mifugo mingine. kuku wamezoeleka kwani hufugwa na watu wengi barani Afrika na kwingineko. Hata hivyo ni watu wachache sana wanao tambua thamani ya kuku. Nchini Tanzania watu walio na kuku ni wengi japo inasadikika kuwa ni asilimia 8.2 tu kati ya wote walio na kuku wanao nufaika kwa sehemu na umiliki wa kuku. Utafiti umeonesha kuwa Watanzania wengi wanamiliki kuku, siyo wafugaji wa kuku kwani kuku wao hujifuga wenyewe. Hii ni kutokana na wengi kati ya wafugaji kufuga kwa mazoea. Ufugaji wa kuku ukifanyika kwa utaratibu mzuri huleta mafanikio makubwa kwa mfugaji. Hauishii kumuwezesha kuishi, bali humtajirisha na kumuweka katika hatua ya mafanikio zaidi kwa kadri ya juhudi zake. Ufugaji wa kuku ni fursa pana inayo weza kutekelezwa na yeyote bila kujali mtaji wake, elimu, mazingira alipo wala hali yake ya kimaisha. Ufugaji wa kuku kibiashara haujawahi kumuangusha yeyote aliye thubutu kuutekeleza kwa malengo na kuendesha kwa ufanisi. Kitabu hiki ni mwongozo sahihi wa namna ya kunufaika na ufugaji wa kuku. Kimebainisha mfumo rahisi na wa kisasa wenye mafanikio makubwa katika ufugaji wa kuku. Changamoto zote zinazo ukabiri ufugaji wa kuku zimetatuliwa katika kitabu hiki. Anza kuyafuata maelekezo yake, unufaike na kutajirika kupitia ufugaji wa kuku. YALIYOMO UTANGULIZI 2 YALIYOMO.. 3 SURA YA 1. 4 MRADI WA UFUGAJI WA KUKU.. 4 MAZAO YA KUKU.. 5 AINA ZA KUKU.. 5 SURA YA 2. 6 KUKU WA ASILI 6 SIFA ZA KUKU WA ASILI 6 AINA ZA KUKU WA ASILI 6 FAIDA ZA KUFUKA KUKU WA ASILI 8 UFUGAJI WA KUKU WA ASILI 8 MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI 8 MAHITAJI MUHIMU KATIKA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI 11 HATUA ZA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI KWA FAIDA. 11 KUCHAGUA KUKU BORA WA KUFUGA. 11 BANDA BORA LA KUFUGIA. 12 UJENZI WA BANDA. 13 KUTUNZA NA KULISHA KUKU KULINGANA NA HATUA MBALIMBALI ZA UKUAJI 14 KULEA VIFARANGA. 16 ULISHAJI WA KUKU.. 18 USAFI KATIKA BANDA LA KUKU.. 21 SURA YA 3. 22 KUKU WA KISASA. 22 KUKU WA MAYAI 22 KUKU WA NYAMA. 22 Tofauti kati ya kuku wa Asili na kuku wa Kisasa. 23 HATUA ZA KUFUKA KUKU WA KISASA. 23 SURA YA 4. 25 UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI 25 Utumiaji wa mashine; 25 MATAYARISHO KABLA YA VIFARANGA KUWASILI 26 UAGIZAJI WA VIFARANGA. 27 MAPOKEZI YA VIFARANGA. 27 ULISHAJI 28 JOTO.. 28 MALEZI YA MITEMBA NA MITETEA. 29 MATUNZO YA KUKU WAZAZI 31 SURA YA 5. 33 UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA. 33 KUFUKA KWA FAIDA HUHITAJI KUZINGATIA HAYA. 33 SURA YA 6. 35 MAGONJWA YA KUKU, KINGA NA TIBA ZAKE. 35 MAGONJWA YA KUKU, KINGA NA TIBA ZAKE KITAALAM.. 36 FAHAMU BAADHI YA MAGONJWA HATARI YASHAMBULIAYO KUKU, UENEAJI WAKE, DALILI, KINGA NA TIBA ZAKE: 37 Sura ya 7. 50 UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KUKU. 50 SURA YA 1 MRADI WA UFUGAJI WA KUKU Nyama ya kuku pamoja na mayai ni hitaji kubwa kote duniani. Nchini Tanzania kunasadikika kuwa kuna kuku wapatao milioni therathini na nne ambao ni wachache ukilinganisha na mahitaji yaliyopo. Kwa mujibu wa shirika la chakula duniani “FAO” mahitaji ya nyama ya kuku kwa mtu mmoja ni kilo 6.8 kwa mwaka ambapo Nchini Tanzania utafiti unaonesha kuwa matumizi ya nyama ya kuku yaliyopo kwa sasa ni wastani wa kilo 0.7 kwa kila mtu kwa mwaka. Hapa utagundua kuwa bado uhitaji wa nyama ya kuku uliopo ni mkubwa kwani kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Watanzania ni zaidi ya million 44. Kwa sababu hiyo ufugaji wa kuku ni fursa pana sana hapa Nchini. Idadi ya wafugaji wa kuku nchi Tanzania ni wengi ambao kimsingi kama wangefuga kwa kuzingatia taratibu za ufugaji, wangelisha kuku siyo Tanzania tu bali wangelisha Dunia. Hatahivyo ufugaji wao ni duni kwani wengi wao wamekuwa wakifuga kwa mazoea. Wanao kuku majumbani mwao lakini hawawajali wala kuwapa nafasi yoyote ya umuhimu kwa upande wa huduma. Hii imepelekea ufugaji wa kuku kuonenaka kuwa ni jambo la kawaida ingawa kwa uhalisia wake ufugaji wa kuku ni mradi, ni kazi, ni ajira na ni maisha kamili ya watu. Mradi wa ufugaji wa kuku una utajiri mkubwa ukifanyika kwa ufanisi. Huhitaji elimu kiasi katika utekelezaji wake, nguvu kiasi na muda wa kutosha. Ni rahisi, unao weza kufanywa na mtu yeyote. Ufugaji wa kuku ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umaskini. Pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujatumika ipasavyo kupambana na umaskini unao wakabiri Watanzania wengi. Kuku wa kienyeji ambao hufugwa na watu wengi wamekuwa wakifugwa bila kupatiwa mahitaji muhimu kama chakula cha ziada, makazi bora, kinga na tiba za magonjwa pamoja na uangalizi! Hali inayo pelekea wafugaji kunufaika na kitoweo tu pamoja na kipato kidogo katika kazi yao ya ufugaji. MAZAO YA KUKU Faida ya kufuga kuku inapatikana katika mazao ya kuku. Mazao ya kuku huweza kumnufaisha mfugaji kwa kuyatumia mwenyewe pia kuuza na kujipatia pesa. Mazao yatokanayo na kuku ni; AINA ZA KUKU Yapo makundi makuu mawili ya kuku; Kuku Wa asili na kuku wa kisasa. katika makundi haya ndimo tunamo pata aina mbalimbali za kuku. Uwepo wa aina za kuku hutokana na muingiliano wa vinasaba pamoja uendelezaji wa kibaiolojia. Katika kuendeleza kuku kibailojia; Wataalamu wa Baiolojia hukutanisha kuku wa aina moja na wa aina nyingine, kutumia vyakula au dawa ili kupata aina bora kulingana na malengo yao. Wataalamu hawa hufanya hivi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao ya kuku hivyo juhudi yao ni kuhakikisha wanapata kuku wanao taga kwa haraka na wanao taga mayai mengi. SURA YA 2 KUKU WA ASILI Kwa namna nyingine huitwa kuku wa kienyeji. Hawa ni kuku wa asili ambao walikuwepo kabla ya kuanza kwa uedelezaji wa ki-baiolojia/teknilojia na upandikizaji wa mbegu. Ni kuku ambao bado wapo katika asili yao. Ni Wastahimivu wa changamoto za kimazingira ikiwa ni pamoja na magonjwa, pia huweza kujihudumia kiasi fulani ikiwa ni pamoja na kujitafutia chakula, kujilinda n.k. Hata hivyo kwa lengo la kuwafuga kwa faida, mfugaji anatakiwa kuwafuga kiaalam na kuwapa huduma zote muhimu ili kunufaika na kazi yake ya ufugaji. SIFA ZA KUKU WA ASILI Kuku wa kienyeji wanazo sifa nyingi