Tenzi za Rohoni 80 – Wamwendea Yesu kwa kusafiwa

Tenzi za Rohoni 80 – Wamwendea Yesu kwa kusafiwa

Tenzi Na. 80

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 80, “Wamwendea Yesu kwa kusafiwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je neema yake umemwagiwa,
Tumeoshwa kwa damu ya kondoo?
Kuoshwa, kwa damu,
Itutakasayo ya kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
Wamwandama daima mkombozi
Na kuoshwa na damu ya kondoo?
Yako kwa msulubiwa makazi,
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?
Atakapokuja Bwana –arusi
Uwe safi kwa damu ya kondoo!
Yafae kwenda mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya kondoo.
Yatupwe yaliyo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya kondoo.
Huoni kijito chatiririka
Na uoshwe kwa damu ya kondoo?


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top