Tenzi za Rohoni 79 – Msalaba Wa Aibu

Tenzi za Rohoni 79 – Msalaba Wa Aibu

Tenzi Na. 79

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 79, “Msalaba Wa Aibu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Msalaba wa aibu,
Ulinipa amani;
Uliniondoa kifungoni,
Nilimotesekea.
Ee, Mwokozi wangu, Yesu
Nitamwendea nani?
Najiweka msalabani,
Nikaoshwe damuni.
Nakupenda Bwana Yesu,
Kwa kunipenda kwako,
Napendezwa nikutumikie
Maisha yangu yote.
Usifiwe Bwana Yesu,
Kwa ulivyonifia,
Aleluya, nakushukuru,
Uliyenikomboa.
Msalaba ulishinda
Nguvu zake adui,
Ili mimi nikombolewe,
Niwe mwana wa Mungu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top