Tenzi za Rohoni 78 – Sioshwi Dhambi Zangu

Tenzi za Rohoni 78 – Sioshwi Dhambi Zangu

Tenzi Na. 78

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 78, “Sioshwi Dhambi Zangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Sioshwi dhambi zangu,
Bila damu yake Yesu.
Hapendezewi Mungu,
Bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa
Dawa ya makosa
Ya kututakasa,
Ila damu yake Yesu.
La kunisafi sina
Ila damu yake Yesu.
Wala udhuru tena,
Ila damu yake Yesu.
Sipati pataniswa,
Bila damu yake Yesu.
Hukumu yanitisha,
Bila damu yake Yesu.
Sipati tumaini,
Bila damu yake Yesu.
Wema wala amani,
Bila damu yake Yesu.
Yashinda ulimwengu,
Hiyo damu yake Yesu.
Na kutufikisha juu,
Hiyo damu yake Yesu.
Twaimba: Utukufu
Una damu yake Yesu.
Milele twaisifu,
Hiyo damu yake Yesu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top