Tenzi za Rohoni 77 – Msalabani Pa Mwokozi

Tenzi za Rohoni 77 – Msalabani Pa Mwokozi

Tenzi Na. 77

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 77, “Msalabani Pa Mwokozi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Msalabani pa mwokozi,
Hapo niliomba upozi,
Akaniokoa mpenzi,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Chini ya mti msumbufu,
Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
Aliniokoa dhambini,
Ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia mtini,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu.
Damu ya Yesu ya thamani,
Huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
Hicho kijito cha gharama,
Leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima,
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top