Tenzi za Rohoni 81 – Chini Ya Msalaba

Tenzi za Rohoni 81 – Chini Ya Msalaba

Tenzi Na. 81

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 81, “Chini Ya Msalaba”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Chini ya msalaba
Nataka simama;
Ndio mwamba safarini,
Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu
Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu
Wakati wa hari.
Hapa ni pema sana,
Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana,
Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa
Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa
Ngazi ya Mbinguni.
Na Yesu msalabani
Walimkemea,
Alikufa niokoke
Niliyepotea;
Naona ajabu sana
Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda,
Nisiyestahili.
Atakayeonana,
Na Yesu Mbinguni,
Njia yake aanzapo
Ni msalabani;
Wokovu upo hapa tu,
Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu
Pamoja na Bwana.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top