Tenzi za Rohoni 49 – Nitwae Hivi Nilivyo

Tenzi za Rohoni 49 – Nitwae Hivi Nilivyo

Tenzi Na. 49

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 49, “Nitwae Hivi Nilivyo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu,naja,naja.
Hivi nilivyo;si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu,naja,naja.
Hivi nilivyo; sioni
Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu,naja,naja.
Hivi nilivyo kipofu,
maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu;
Bwana Yesu,naja,naja.
Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu,naja,naja.
Hivi nilivyo;mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu,naja,naja.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top