Tenzi za Rohoni 48 – Naweka Dhambi Zangu
Tenzi Na. 48
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 48, “Naweka Dhambi Zangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Naweka dhambi zangu
Juu yake Bwana
Kuziondoa, kwangu
Hulemea sana;
Na uaili wangu
Ameuondoa;
Dawa yangu ni damu,
Kwa hiyo napoa.
Na uhitaji wangu
Nitamjuvisha
Kwa upungufu wangu
Yeye anatosha;
Majonzi yangu yote
Na mizigo yangu,
Atachukua vyote
Yesu Bwana wangu.
Na roho yangu nayo,
Imechoka sana;
Namletea hiyo
Ilindwe na Bwana;
Ni jema jina lake,
Nalo lapendeza,
Imanweli na kwake
tutalitukuza.
Natamani daima
Niwe kama Bwana,
Mpole, tena mwema,
Wa mapenzi sana;
Zaidi natamani
Kwenda kwake juu,
Nikaone mbinguni
Enzi yake kuu.