Tenzi za Rohoni 50 – Yesu Nakupenda, U Mali Yangu

Tenzi za Rohoni 50 – Yesu Nakupenda, U Mali Yangu

Tenzi Na. 50

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 50, “Yesu Nakupenda, U Mali Yangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
Mawanda mazuri, na masikani
Niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top