Tenzi za Rohoni 41 – Yesu Aliniita

Tenzi za Rohoni 41 – Yesu Aliniita

Tenzi Na. 41

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 41, “Yesu Aliniita”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Yesu aliniita, “njoo,
Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze
Kifuani mwangu.”
Nilikwenda kwake mara,
Sana nilichoka;
Nikapata kwake raha,
Na furaha tena.
Yesu aliniita, “njoo,
Kwangu kuna maji,
Maji ya uzima, bure,
Unywe uwe hai, “
Nilikwenda kwake mara
Na maji nikanywa:
Naishi kwake, na kiu
Kamwe sina tena.
Yesu aliniita, “njoo,
Dunia ni giza,
Ukinitazama nuru
Takung’arizia.”
Nilikwenda kwake mara
Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga
Safarini mwangu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top