Tenzi za Rohoni 42 – Kivulini Mwa Yesu
Tenzi Na. 42
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 42, “Kivulini Mwa Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Kivulini mwa Yesu kuna Kituo:
Kituo mbali na hamu, kituo kilicho tamu.
Kivulini mwa Yesu kuna kituo;
kivulini mwa Yesu kuna kituo;
Raha tu, mle; amani tupu,
Furaha tele; kivulini mwa Yesu
Raha tu, mle; amani tupu,
Furaha tele; kivulini mwa Yesu.
Kivulini mwa Yesu nina amani
Iliyopita fahamu, tena itakayodumu.
Kivulini mwa Yesu, nina furaha;
Furaha yenye fahari, ya kueneza habari.