Tenzi za Rohoni 109 – Nitaimba Na Yesu
Tenzi Na. 109
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 109, “Nitaimba Na Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Nitaimba ya Yesu,
Kwa rehema zake,
Baraka nyingi sana
Nimepata kwake;
Nitaimba ya Yesu,
Sadaka ya Mungu,
Alimwaga damu
Ukombozi wangu.
Nitaimba ya Yesu
Hapa siku zote,
Nitakapokumbuka
Vyema vyake vyote;
Nitaimba ya Yesu
Hata mashakani,
Yeye atanilinda
Mwake ubavuni.
Nitaimba ya Yesu
Niwapo Njiani;
Takaza Mwendo, hata
Nifike Mbinguni;
Nikiisha ingia
Mlangoni mle,
Yesu nitamwimbia
Mbinguni milele.