Tenzi za Rohoni 110 – Mapya Ni Mapenzi Hayo

Tenzi za Rohoni 110 – Mapya Ni Mapenzi Hayo

Tenzi Na. 110

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 110, “Mapya Ni Mapenzi Hayo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tunayo,
Saa za giza hulindwa
Kwa uzima kuamshwa.
Kila siku, Mapya pia
Rehema, wema, na afya,
Wokofu, na msamaha,
Mawazo mema, furaha.
Tukijitahidi leo
Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza.
Mambo yetu ya dunia
Mungu atayang’aria,
Matata atageuza
Yawe kwetu ya Baraka.
Yaliyo madogo, haya
Mungu tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi
Huvuta kwake zaidi.
Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top