Kiswahili Form Two Notes – Utungaji wa Kazi za Fasihi Simulizi

Maelezo haya ya Kiswahili Form Two yanahusu Utungaji wa Kazi za Fasihi Simulizi. Yamepangwa katika sehemu zilizo wazi ili kurahisisha kusoma, kuelewa na kufanya marudio.

Kazi za fasihi simulizi hazikutokea tu, zilitungwa. Mtu fulani alikaa na akatunga kazi fulani ambayo inajulikana katika jamii. Katika mada hii utajifunza kanuni mbalimbli zinazohusika na utunzi wa kazi za fasihi simulizi. Pia utapata fursa ya kujifunza jinsi ya kutunga kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile ngonjera, methali , nahau, vitendawili na kazi nyingine. Utajifunza

pia kanuni zinazoongoza utunzi wa kila kazi ya fasihi simulizi.

Mashairi

Kanuni za Utungaji wa Mashairi

Fafanua kanuni za utungaji wa mashairi

Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna

milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja. Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje — je ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni

mlemavu wa macho?

Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?

Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini? Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje — ni chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?

Kusi

je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki — je, iko chini au juu (kelele)?

Uzoefu wa Mwandishi

Uzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu. Mwandishi ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni matatizo gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani umekutana nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011) kuna baadhi ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana nailoni na je kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?

Uchunguzi/utafiti

Uchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa. Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa wasomaji wa kazi zake. Uchunguzi ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika — anatembeaje, anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na wenzane na mazingira yake? | Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.

| Mwandishi baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi yake. Hapa sisi tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika hatua ya utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya hapo tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo yatatuwezesha kutunga mashairi.

Dhana ya shairi

Shairini kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti | za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa_huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.

Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana halisi na | burudani. ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi ijapokuwa hazikuandikwa.

Mashairi yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo kadhaa yanayotakiwa kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:

1. Beti—Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.

2. Vina — Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti ileile mwishoni mwa

sentensi.

3. Mizani — Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.

4. Kituo — Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo vya aina tatu:Kituo cha bahari —

| ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti;Kituo cha kimalizio— ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi

| ubeti;Kituo nusu bahari—ni mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na

nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti. | Katika mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe na maana | kamili.

Vipengele vya fani katika mashairi

| Vipengele vya fani katika shairi ni pamoja na:

© Jina / anwani

Mandhari Wahusika Muundo ~tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k

Mtindo — pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa

mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia. Vipengele vya Maudhui kati mashairi

Vipengele vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo, mtazamo, na dhamira za mwandishi.

Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza, kufundisha,

kuburudisha, kukosoa, na kadharika.

Baada ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza. Kuigiza Ngonjera

Igiza ngonjera

Katika kuigiza ngonjera muigizaji hana budi kuzingatia fani yenye kanuni zifuatazo; mtindo wa mashairi ya kimapokeo, muundo wa mashairi ya kimapokeo wenye mizani, vina, vipande, mishororo na beti, kuteua mandhari kutegemeana na mada, kuwepo kwa wahusika wawili au

zaidi au makundi mawili au zaidi na matumizi ya lugha ya kishairi.

Maigizo

Kanuni za Utungaji wa Maigizo

Elezea kanuni za utungaji wa maigizo

Maigizo ni tendo la kuiga sura, tabia, matendo na mazungumzo ya watu au viumbe wengine

yaani kuiga jinsi walivyoumbwa, wanavyotembea, wanavyovaa, Wanavyosema n.k

Kanuni na hatua za kutunga maigizo

1. Kuchagua wazo, tendo, visa au tukio la kuigizwa:Ni lazima jambo hilo liwe na uzito,

umuhimu au athari fulani katika jamii. Matukio hubainika kutokana na utafiti. Matukio

yanayoweza kuwa kiini cha kutungiwa maigizo ni kama vile matumizi mabaya ya simu za mkononi, mitindo ya mavazi, madhara ya uganga wa kienyeji, madhara ya UKIMWI

nk.

v

Kuchagua muktadha au mahali pa kutendeka kwa jambo:Muktadha waweza kuwa

ofisini, shuleni, kijijini, mjini, barabarani, kwenye daladala n.k

a ereerrera

Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la kuigizwa:Hapa mtunzi anaweza kutumia fumbo, vichekesho, historia, tanzia n.k. Inashauriwa mtunzi kuchanganya mbinu ili kuongeza mvuto. 4. Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo:Maudhui hujikita katika migogoro | au mivutano. Suluhisho la mivutano hupatikana pale migogoro inapofikia kilele. Kwa mfano jamabazi sugu anapokamatwa. | 5. Kuweka mpangilio wa maonyesho:Maonyesho hujumuisha vitendo na_hoja zinazokamilisha sehemu inayobeba aina moja au zaidi ya maudhui. Sehemu kadhaa nazo hukaa zikajenga kitendo ambacho hubeba jambo mojawapo muhimu. Katika migawanyo

hii yapasa mtunzi atunge kauli na vitendo vinavyoandamana navyo.

6. Kubuni wahusika na kuweka aina au idadi yao kulingana na matukio:Mtunzi

anashauriwa kutumia wahusika wanaohitilafiana. Kwa mfano wazee, vijana, wanawake, | wanaume, wanene, wafupi n.k. Mtunzi akishawateua anaweza kuwatungia kauli na zamu za matendo katika schemu mbalimbali.

| 7. Ni muhimu pia kwa mtunzi kuwaumba wahusika wake na kuamua maleba yao:Uamuzi huu yapasa ufanywe kwa kuzingatia mazingira. Kwa mfano siku hizi sio lazima wahusika wazee kuvaa ngozi, kutumia mkongojo na kuvuta mtemba.

8. Urefu wa maigizo ni suala la kuamliwa kutegemea tukio

9. Kutunga maelezo kuhusu mandhari:Maumbile ya wahusika na vitendo vyao, ni

muhimu kuelezwa katika mabano.

| 10. Kuandika maigizo na kuhariri:Ni_ muhimu kutumia lugha ya kimazungumzo

inayovutia, yenye kuleta taharuki na yenye utamu unaoeleza maadili kwa mnato.

Maelezo Ya Ziada

– Sanaa ni mali ya jamii ya kizazi kijacho kitatumia mali hizi zilizotumiwa kujifunza, kuburudika, na hata kugundua sanaa zaidi kwani tayari wana msingi fulani wa kuanzia.

UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Kwa kawaida mshairi anapotunga shairi / wimbo hutoa hisia yake au maoni yake juu ya jambo fulani. Mambo hayo hutolewa kufuatana na jinsi anavyoliona jambo lile na anavyoamini kuhusu jambo lile. Hii ina maana kwamba maoni yale hutolewa kulenga na imani ya mshairi mwenyewe. Imani ya mshairi ndiyo inayojenga msimamo wake katika maisha, yaani falsafa yake.

Mtunzi yeyote katika ushairi, utunzi wake huwa umezingatia vipengele viwili muhimu navyo ni fani na maudhui.

Kwa ujumla mtunzi yeyote wa tanzu ya fasihi simulizi huzingatia vipengele hivi viwili katika utunzi wake.

Kanuni Za Utunzi Wa Ushairi Wa Fasihi Simulizi

Maudhui

– Katika kipengele cha maudhui mtungaji wa mashairi anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo katika kufanikisha lengo la utunzi wake.

Lengo la mshairi

– Kabla hajaanza kutunga shairi lazima ujue sababu za kutaka kueleza hayo unayo taka kueleza kwa maana ya kwamba lazima uwe na jambo lililokusukuma kutunga wimbo au shairi.

– Mshairi anapotunga huwa na kitu maalum akisemacho

– Huwa na ujumbe anakusudia kuwasilisha kwa jamii yake

– Kuelewa vizuri jamii aliyoiandikia

– Mtunzi wa ushairi asitunge bila kuwa anamkusudia mtu au watu fulani. Watu hao waweza kuwa marafiki, watawala, jamaa, maadui au yeye mwenyewe n.k.

– Utakapo mfahamu unaye muandikia itakusaidia kujua utunzi wake kwa sababu utajua imani na taratibu mbalimbali za maisha ya huyo mtu na hii itakufanya utunge vizuri kazi yako na humuathiri vilivyo mlengwa wako.

Kujua mipaka ya uhuru wa uandishi wako

– Mwandishi yeyote huweka mipaka katika uandishi wake .Kwa hiyo mtunzi yoyote Yule atake au asipende hujikuta amewekewa mipaka katika utunzi wake. Hivyo Kama mtunzi yakupasa utambue mipaka yako kwani pasipo kufanya hivyo utasababisha matatizo. Iwapo utavuka mipaka vizuri kutasaidia kuyaandika yale unayoyataka kwa ustadi na kufikisha ujumbe utakao kusudiwa bila matatizo.

Kuoanisha dhamira na wakati

– Ni muhimu mtunzi kuandika jambo hilo ambalo anafikiri jamii yake inahitaji kwa wakati huo. Mfano mtunzi anaweza kuandika juu ya uongozi mbaya, UKIMWI, madawa ya kulevya kwani mambo hayo ndiyo yanayo tugusa katika jamii zetu.

– Kwa hiyo kama mtunzi ataandika mambo ambayo yanaenda na mahitaji ya jamii kwa kipindi hicho basi atapata hadhira kubwa kuliko akiandika mambo yaliyopitwa na wakati. Kwa hiyo basi mtunzi lazima awe na jambo kuu moja ambalo analitafutia ujumbe mbalimbali na mawazo madogo madogo ambayo yatakayo kamilisha ujumbe huo .

Fani

Mambo muhimu ya kuzingatia

Kuoana – Utungo wa ushairi ni masimulizi ya tukio fulani au maelekezo juu ya jambo fulani. Hivyo basi ni kwamba masimulizi au maelezo hayo yanahitaji mtiririko wenye mawazo mazuri yenye kuoana

• Utungaji ambao hauna mpangilo mzuri huwa na matatizo mbalimbali kama vile kukosa kuelewa kile asemacho.

• Upangaji mbaya wa mawazo husababisha shairi kukosa ladha na hivyo msikilizaji hukosa hamu ya kusikiliza

Kutotumia mitindo inayofaa

– Uchanganuzi wa aina ya shairi atakao tumia mtungaji unategemea sana dhamira iliyo kusudiwa pamoja na lengo alilonalo msanii mwenyewe.

Mfano:-

– Unapo taka kuzungumza mambo ya kihistoria kwa urefu na upana inabidi atumie utam wa utenzi kuliko wimbo au ushairi kwani tenzi inaweza kutungwa beti nyingi kulingana na kitu kinacho zungumziwa

Utenzi wa lugha

– Lugha ni kipengele muhimu sana katika ushairi. Mtunzi wa ushairi katika kipengele cha lugha ni lazima awe makini kwani lugha isipo kuwa tamu husababisha hata maudhui kuwa chapwa. Mtunzi lazima azingatie mambo yafuatayo katika kipengele cha lugha.

1. Lugha ya kishairi

– Ushairi una lugha yake tofauti na lugha itumiwayo katika mazingira mengine ya kawaida kwani lugha ya ushairi ni ya kutumia maneno machache ya mkato na siyo mengine.

2. Matumizi ya picha

– Hii husaidia kuvuta taswira ya mambo yanapo ongelewa na kukamata akili ya msikilizaji kwa namna ya ajabu. Pia husaidia sana kuvuta hisia na kuleta mguso wa hali ya ajabu na hisia za juu kwa msikilizaji.

3. Matumizi ya tamathali za semi

– Hizi hupanua au hubadilisha maana ya halisi au ya kawaida za maneno ili kuleta maana maalumu iliyo kusudiwa na mtunzi . Mtunzi wa shairi atakapozijenga tamathali zake vizuri huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayo elezwa huiburudisha na kuzindua akili ya msikilizaji wa shairi na huacha athari ya kudumu katika hisia ya mawazo yake.

– Tamathali zinazotumika zaidi katika ushairi ni tashbiha, tashhisi, mbalagha, kejeli, sitiari n.k. Hivyo mtunzi wa shairi lazima atumie tamathali kujenga kazi yake.

4. Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa

– Kuna mbinu nyingine za kisanaa zinazo karibiana na tamathali za semi ambazo hutumika nsana katika utunzi wa mashairi. Mbinu ambnazo hutumiwa sana na ushairi ni takriri, tanakali sauti , ridhimu ( mapigo asilia ya lugha ) n.k. Kwa hiyo wakati wa kutunga msanii lazima azingatie mbinu kama hizi.

5. Matumizi ya nahau na misemo

– Hivi ni viungo muhimu katika lugha ya ushairi na kufanya lugha ya msanii au mwandishi fulani kuwa na mivuto mikubwa ya kisanaa, hivyo ni muhimu kuzingatia matumizi ya nahau na misemo.

6. Matumizi ya methali

– Methali hutumiwa sana na wasanii kwani hutumiwa sana katika kupitisha hekima na busara kwa jamii na pia hutumika kujenga na kupamba lugha.

7. Lugha ya wahusika

– Tunapozungumzia kuwa kuna lugha ya wahusika ina maana kuwa kama msanii amekusudia kutoa maonyo basi inambidi atumie lugha ya maonyo . Vilevile kama atatumia hadhira maalum basi lugha lazima ieleweke na hadhira hiyo.

8. Kuzingatia kanuni za uandishi

– Kuna kanuni ambazo zinatakiwa kufuatwa hasa unapotaka kutunga mashairi ya kimapokeo ambazo ndizo nguzo hasa za ushairi na pia kuna mambo mengine yanayo takiwa kufuatwa katika kutunga mashairi.

Kanuni za utunzi wa mashairi ya kimapokeo

1) Vina

– Katika ushairi vina ni ile mizani ya kati na ya mwisho yenye kufanana katika kila mstari wa ubeti. Katika tabia aghalabu vina hufuatana katika kila mishororo mitatu ya mwisho inaweza kubadilika.

2) Kituo

– Huu ni mstari wa mwisho katika kila ubeti wa ushairi. Kituo cha mstari kinaweza kuwa kimalizio au kiini kituo kinapo kuwa kimalizio kinatumika kulifunga na kukamilisha wazo moja katika kila ubeti. Na kinapokuwa kiini kina jitosheleza katika kila mwisho wa ubeti na kutaja kwa muhtasari jambo muhimu linalozungumziwa.

3) Kipande

– Hiki ni kisehemu kimojawapo katika visehemu viwili au zaidi katika kila mstari kutegemea na mtunzi mwenyewe alivyo amua kutunga kazi yake.

4) Mizani

– Ni jumla / idadi ya silabi zilizomo katika kila mstari wa ubeti mizani husaidia kuleta mapigo katika shairi na kufanya liweze kuimbika.

– Mara nyingi shairi la kimapokeo huwa na mizani 16 na lazima ifanane katika kila kila ubeti wa shairi lakini ushairi wa fasihi simulizi si lazima mizani ifanane sana.

5) Ubeti

– Hiki ni kifungu chenye kuleta maana kamili katika jumla ya vifungu ulivyo navyo kwenye shairi na ubeti hubeba wazo kamili katika shairi.

6) Urari

– Pia mtunzi lazima azingatie kuwa na urari na mawazo kati ya mstari na mstari au ubeti na ubeti kwani kuna baadhi ya watunzi hukosea au katika kazi zao kunakuwa hakuna urari wa mawazo au mawazo hayaoni.

7) Utoshelezi

– Mtunzi yeyote wa shairi la Kiswahili ni lazima azingatie utoshelezi wa ubeti kwani ni lazima kila ubeti ujitosheleze kimaana( ujumbe kabla hujaingia kwenye ubeti wa pili msomaji anapaswa awe ameelewa kitu gani kilichokuwa kinaongelewa kwenye ubeti wa kwanza na pia mshororo nao inabidi uwe ni wenye kiujumbe.

8) Kuwa na maana

– Pia shairi ni lazima liwe na maana kwani hili pia ni jambo la msingi katika ushairi kwani mtunzi anaweza kufuata kanuni zingine zote lakini bado shairi lake linaweza lisieleweke kwani alikuwa anataka hadhira yake ijifunze nini.

– Vilevile mtunzi anaweza akagundua beti Kama kumi lakini shairi linakuwa halina maana na msanii mwingine akafunga hata beti moja tu na shairi lake linakuwa na maana kamili na kuwa na ujumbe unaoleweka.

9) Muwala

– Ni ufuatanisho wa habari toka ubeti hadi ubeti. Mfano shairi lenye beti nane linaweza kuleta zama ukaona ubeti wa nne ungekuwa wa pili na wa pili labda ungekuwa mahali fulani au usinge kuwepo kabisa kutokana na mtiririko ulivyo kuwa. Haya yote ni katika kufanya miwala iwe mizuri katika shairi na hiyo ni moja ya kazi ngumu katika kutunga shairi la Kiswahili

10)Msisitizo

– Hii ni hali ya kushadadia kwa kiini cha jambo au dhamira kuu katika utungo huo kama tulivyo kwisha ona msisitizo katika shairi laweza kuwa wima au ulalo

– Baada ya kuona hizo kanuni za mtunzi na shairi tuangalie mambo mengine ambayo pia ni muhimu katika utunzi wa shairi ili liweze kuwa bora au zuri zaidi mambo hayo kama;-

I. Kutorudia maneno

– Shairi litapungua utamu kwa kurudia maneno. Msanii anaporudia neno moja katika kila ubeti husababisha shairi kukosa ladha na utamu, pia mtunzi huonekana kama hana ujuzi wa lugha.

Lakini kuna mashairi ya msisitizo ambayo toka ubeti wa kwanza mpaka wa mwisho huanza na neno hilo basi kama neno huanza na shida basi katika kila ubeti huanza na neno hilo hilo hiyo siyo kurudia maneno bali ni mtindo wa msanii.

II. Kichwa cha shairi

Kichwa cha shairi ni muhimu sana katika kufikisha ujumbe kwa msikilazaji kwa hiyo kama shairi halina kichwa basi linakuwa sio tamu. Shairi ambalo ni bora ni lile linalo kuwa na kichwa

1. Kutochanganya dhamira

Pia unapo changanya dhamira mbili au zaidi katika shairi moja hilo linakuwa shairi baya kwani unapo andika shairi inabidi uende na dhamira moja kuanzia ubeti wa kwanza mpaka wa mwisho ndipo shairi linapendeza sana na hii husaidia kueleweka kwa dhamira ya shairi.

1. Kunga

Siri ya shairi ni kulihifadhi lisiwe mbali sana. Ni kwamba mtunzi anapotunga inabidi asitumie lugha ya kashfa au ya matusi. Anaweza kutumia lugha ya mafumbo ili aweze kuyafumbua.

Matumizi ya tamathali za semi

– Hizi hupanua au kubadilisha maana za dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta maana maalum iliyo kusudiwa na mtunzi . Mtunzi wa shairi atakapo zijenga tamathali zake huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayoelezwa, pia huburudisha na kuzindua akili ya msikilizaji wa shairi na kuacha athari ya kudumu katika hisia na mawazo yake.

– Tamathali zinazo tumika katika ushairi ni tashbiha, tashihisi, kejeli, sitiari, n.k. Hivyo mtunzi wa shairi lazima atumie tamathali katika kujenga kazi yake.

Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa

– Kuna mbinu nyingine za kisanaa zinazo karibiana na tamathali za semi ambazo hutimika sana katika utunzi wa shairi . Mbinu ambazo hutumiwa sana na ushairi ni takriri, tanakali sauti(onomatopea), rithimu, mapigo asilia ya lugha n.k. kwa hiyo wakati wakutunga msanii lazima azingatie mbinu kama hizi.

Matumizi ya nahau na misemo

– Hivi ni viungo muhimu katika lugha ya ushairi na huifanya lugha ya msanii au mwandishi fulani kuwa na mvuto mkubwa wa kisanaa. Hivyo ni muhimu kuzingatia matumizi ya nahau na misemo.

Matumizi ya methali

– Methali hutumiwa sana na wasanii katika kupitisha hekima na busara kwa jamii na pia hutumika kujenga kejeli kwa kupamba lugha

Utungaji Wa Maigizo

– Mtungaji yeyote anapotaka kutunga maigizo kuna vipengele mbalimbali ambavyo jamii inapitia vizuri kazi yake na akaweza kubuni mbinu ambazo zitaifanya kazi yake ipendeze na kuvutia kwa hiyo itakidhi mahitaji ya jamii husika kwa kipindi hicho

Vipenngele muhimu vyaa kuzingatia katika utunzi wa maigizo

(a) Lengo la mtunzi

– Mtunzi lazima aandike maudhui yenye umuhimu katika jamii na yanayoendana na wakati. Msanii mzuri inabidi apange maudhui yake hata kama yakiwa yanahusu Tanzania ya zamani lazima yawe na umuhimu katika Tanzania ya leo . Pia anaweza akazungumzia masuala tofauti tofauti ambayo yanaleta maendeleo kwa jamii

(b) Hadhira inayoandikiwa.

Mtunzi lazima ajiulize anaandika kwa hadhira gani kwani hadhira atakayo iandikia ndiyo itakayo amua usanii ni nini na vipi jambo hili ni muhimu kwa mtunzi kwa sababu kufaulu au kutofaulu kwa igizo hutegemeana na hadhira yako itakavyo pokea hilo igizo litakalo oneshwa jukwaani. Msanii pia inabidi afahamu mawazo ya hadhira yake. Juu ya jambo analotaka kuwasilisha kama ni tofauti na mtazamo wake basi atumie mbinu itakayo shawishi wakubaliane nayo.

(c) Utenzi wa vitendo.

– Msanii anapotunga igizo lazima achague matendo ambayo yatasaidia kulijenga wazo lako. Wazo moja linalotokeza huwakilishwa na matendo mengi ambayo yatasaidia kufikisha ujumbe vizuri vile ulivyokusudiwa hadhira yake ipate kujifunza. Dhamira yake kuu ndiyo itakayo muwezesha achague matendo ya aina fulani.

(d) Ujengaji wa wahusika

– Wahusika wa maigizo inabidi wajengwe kutokana na msukumo na migongano iliyomo katika igizo. Maneno, mawazo na matendo yao yapate chanzo kutokana na migogoro hiyo. Kwa namna hiyo wahusika watapata uhalisia na kuvaa uhusika wa kuaminika katika jamii waliyotoka.

(e) Uteuzi wa maneno

– Mtunzi wa igizo anapaswa kuchagua maneno kwa uangalifu kwa sababu wakati mwingine mtunzi huwapa wahusika wake maneno mengi kiasi kuwa igizo linakuwa na maneno matupu kuliko vitendo kwani matendo yakiwa yamejengwa vizuri huleta maana husika kwa hadhira na maneno machache hupelekea igizo kuwa zuri na la kuvutia

(f) Uteuzi wa misukumo

– Msanii anapaswa achague misukumo itakayoweza kusababisha mitazamo isitokee. Na ili jambo litokee inabidi ajenge pande zote ziwe na misukumo yenye nguvu ambayo italeta matokeo na kama upande mmoja ni dhaifu basi hakuna jambo litakaloweza kutokoea.

(g) Matendo jukwaani

– Mtunzi anatakiwa achukue matendo ambayo yanaweza kuoneshwa katika jukwaa. Igizo lolote haliwezi kukamilika bila kuoneshwa jukwaani ili liweze kuonekana kwa hadhira.

– Mtunzi inabidi achague matendo ambayo yanaweza kuonesheka huku yakiambatana na mbinu zingine.

Uigizaji Wa Maigizo Jukwaani.

Maigizo yanapo kuwa yanaoneshwa kwenye jukwaa huonesha matendo ya binadamu na maisha wanayoishi kila siku iitwayo leo

Katika uigizaji wa maigizo mambo muhimu ya kuzingatia ni :

a) Jukwaa

– Katika maigizo lazima kuwe na jukwaa la kuigizia ambalo ni kitu muhimu katika tanzu hii. Zamani maigizo yalikuwa yanaigizwa nje lakini siku hizi hutumia majukwaa ya ndani.

– Hii ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia hata hilo jukwaa la ndani bado ni dhiki kuigiza katika jukwaa hilo

b) Mazungumzo

– Vile vile mazungumzo ya wahusika ni muhimu sana tofauti na maelezo ya mtunzi kwani husababisha igizo kuwa zuri na kuvutia machoni mwa watazamaji.

c) Mavazi

– Mavazi ya wahusika ni muhimu sana katika maigizo. Hii ni kwa sababu wahusika wanapo igiza wanatakiwa kuonesha watu walivyo wanavyoishi katika kipindi fulani cha historia au watakavyo ishi siku zitakazokuja.

– Hayo mavazi wanayovaa yaendane na uhalisia wa maisha ya jamii hiyo na kile kilichoigizwa.

– Pia maleba huonesha bayana tofauti za kitabaka zilizopo katika jamii. Kazi ya upambaji hufanywa na mpambaji wa jukwaa au mkurugenzi wa maigizo.

d) Vifaa vya kuigizia

– Vifaa vinavyotolewa na mtunzi kwa ajili ya kutumika jukwaani mara nyingi huwa na umuhimu. Mtunzi anatakiwa ahakikishe kwamba vifaa anavyo tumia mhusika aoineshe halisi ya lile jambo analowasilisha.

Mfano:-

– Igizo linataka kuonyesha watu wanavyoishi vijijini .

– Hivyo basi ni muhimu vifaa vinavyo teuliwa viwe na uhusiano barabara na uhalisia wa jamii iliyo teuliwa.

e) Jinsi ya kuigiza

– Wahusika wanatakiwa watende vitendo kwa hisia kuliko maneno. Mhusika anatakiwa afanye hivyo kama kweli yamemtokea yeye (kumgusa yeye mwenyewe) katika maisha yake kwa kufanya hivyo atakuwa amefanikiwa kuvaa uhusika na watazamaji wanapata hisia na kuzama katika kulitafakari hilo igizo.

Mfano :-

– Mtu anatakiwa aigize kama ana huzuni lakini yeye anatabasamu

f) Mpangilio wa maigizo

– Katika maigizo huwa na maonesho mbalimbali ambayo huweza kujisimamia yenyewe lakini wakati mwingine huingiliana na maonesho mengine kwa ajili ya kukamilishana. Mawazo hayo huweza kupangwa katika sehemu mbili mpaka saba na katika sehemu moja katika maudhui kadhaa hupatikana na h ndio hutupatia vitendo vya wahusika.

– Kwa hiyo kitendo kimoja hutupelekea jambo fulani na mambo yanapokuwa mengi sharti kuwa na uwiano katika kujenga migogoro mpaka kufikia kilele na kupata suluhisho la hiyo migogoro.

g) Maigizo katika maigizo

– Tanzu hii ya maigizo wakati mwingine inawezekana kukawa na igizo ndani ya igizo. Katika maigizo ya namna hii kuna igizo ndani ya igizo moja ambalo linakuwa ndani ya akili ya wahusika na mtunzi hupandisha jukwaani na kuoneshwa au watazamaji huingiziwa katika upande wa upili ambalo huwa na mambo yanayo shughulikiwa.

Mfano :-

– Mtu aliye kuwa maskini anakuwa tajiri mwanafunzi anakuwa daktari au profesa na kuonesha matendo ya huyo profesa na wakati ikiendelea hivyo moja huwa limegandishwa.

h) Mwisho wa mchezo.

– Mwisho wa uigizaji suluhisho linaweza kupatikana au lisipatikane kipindi cha nyuma mchezo ulikuwa hauishi hii ni kwasababu walikosa njia mbadala ya kuondokea jukwaani lakini siku hizi watunzi mbalimbali wanaweza kutoa masuluhisho na wakati mchezo unaishia waigizaji huondoka jukwaani kwa amani

Kuigiza Ngonjera.

– Ngonjera ni aina ya ushairi zinazowasilishwa kwa kutumia mazungumzo ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi.

– Jambo kubwa kabisa katika ngonjera ni kwamba zenyewe husemwa haziimbwi kifani na kimaudhui hufuata taratibu zote za ushairi

Vipengele muhimu vya ngonjera

(i) Dhamira maalumu.

– Ngonjera huwa na dhamira maalum yaani hujibu swali. Ngonjera hii imeandikwa juu ya nini? Je ina usemi kwa waangaliaji wake?

(ii) Wahusika

– Pia ngonjera huwa na wahusika inaweza ikawa na wahusika wawili au zaidi mpaka wahusika wanne. Mfano inaweza kuwa na wahusikia wawili, mmoja mjuaji na mwingine ni maalum asiyejua kitu chochote na mwisho wa ngojera yule maalumu anakuwa amekubaliana na yule mjuaji.

– Watunzi wengi siku hizi wameongeza wahusika zaidi ya wawili kwa sababu mchezo hauwezi kuchezwa bila wahusika kwa maana wao ndio wana himili hisia zao wanaakili na kutimiza hizo akili zao katika kutatua migogoro inayo wakabili.

– Waandishi hugawanya wahusika wao katika sehemu mbili mhusika mkuu na wahusika wadogo. Mara nyingi mhusika mkuu huwa mwema na wahusika wadogo wadogo huwa wabaya lakini mtindo huo sio mzuri ni dhaifu.

(iii) Migogoro

– Moyo wa mchezo wowote wa kuigiza uwe ni ngonjera au maigizo upo katika migogoro inayojengwa na mjuaji anajibu kumdokeza yule asiyejua ili aweze kujua na mgogoro upate kuisha

– Mgogoro unaweza kuwa kati ya mtu na mtu, mke na mume, au mtu binafsi au migogoro ya kisiasa n.k.

– Migogoro inafanya ngonjera ziwe na uhai na ziweze kutafakariana kiakili na kuamsha shauku ya utafiti unao ambatana na fikra.

– Kwa hiyo uti wa mgongo wa ngonjera ni migogoro na ngonjera nzuri zaidi iambatane na vitendo ili kuleta uhai zaidi na huleta msisimko katika uonyeshwaji.

(i) Lugha :

– Lugha ya ngonjera ni rahisi, sanifu na ni ya kisasa. Lugha ya ngonjera hushawishiwa na wakati tuliopo matatizo yanayo ambatana na mazingira pamoja na siasa ya nchi.

– Ngonjera huongeza msamiati katika lugha ya Kiswahili kwa wanao zisoma, kuzicheza, na pia kutilia mkazo katika lafudhi na kutamka vyema maneno ya Kiswahili.

– Fani hii inawasaidia wachezaji pia waangaliaji kukuza msamiati wao lafudhi. matamshi na ukakamavu katika kutumia lugha sanifu na rahisi kwa umma.

(ii) Mazungumzo ( mjadala )

– Ngonjera huwa na watu ambao hujibizana. Mhusika mmoja hutoa hoja ili ajibiwe na mwingine na mwandishi anayepaswa amwachie mhusika wake aonekane kwamba maneno anayoongea ni ya kwake mwenyewe siyo ya mwandishi. Na mhusika inambidi maneno anayo tumia yaendane na kile anachokiwakilisha. mfano: Daktari mvivu. Pia mjadala utusaidie kumjua mhusika tabia yake hisia zake mawazo yake, mazingira yake, wakati anaozungumzia na kutuonesha hali ya mchezo kiujumla.

(iii) Muundo

– Ngonjera Ina muundo ambao kama wa shairi ingawa kuna tofauti ndogondogo zinazo tofautisha ngonjera na shairi. Kutokana na muundo tunaona visa vinavyotiririka, vinavyojengwa kufikia kukua mpaka mwisho.

– Lazma mawazo ya mwandishi wa ngonjera yafuatane hatua kwa hatua yawe na mantiki na yaliyo na mtiririko wa fikra zenye kueleweka.

(iv) Vitendo

– Mara nyingi taswira au vitendo huanza kabla ya maneno vivyo hivyo misisimko inayotolewa na silka zilizojificha kama huzuni, furaha, huanza kuonekana kabla mtu hajaanza kuongea. Matendo yanatusaidia kufahamu anachofanya mhusika kwa sababu matendo na muondoko wa kulima ni tofauti na ya mwalimu n.k kwani hutofautiana jinsi ya kutumia macho, mikono, uso na hata jinsi ya kuweka mkazo na mlegezo.

– Vitendo hutasaidia kujua dhahiri dhamira za ngonjera yenyewe

(v) Jukwaa na vitu vinavyoonekana wakati wa kufanya ngonjera

– Tanzu yoyote ya fasihi simulizi huwa na mahali ambapo inatendekea na huitwa mandhari.

– Katika ngonjera pia huwa na mandhari ambayo yaweza kuwa shambani sokoni ukumbi wa mkutano kijijini au ndani ya nyumba, ofisini n.k. au inaweza kuchanganya mandhari mbili au zaidi kutokana na mwandishi alivyoamua kujenga kazi yake.

– Kwenye ngonjera kitu ambacho hutusaidia kujua mandhari ni maneno ya mhusika mwenyewe na maelezo ya mwandishi au kama linachezwa katika jukwaa ambalo jamii inaweza kuona maigizo hayo.

(vi) Mavazi ya wahusika wa ngonjera

– Mavazi ya wahusika katika ngonjera ni muhimu sana kwa sababu yatasaidia katika kufikisha ujumbe wa hadhira husika.

– Na pia yatatusaidia kutupa mwanga zaidi na kujua wahusika wetu na pia kutupa kazi na nafasi ya wahusika wa ngonjera hiyo.

– Na vilevile hutusaidia kujua vipindi mbalimbali ambavyo jamii imepita mfano; mavazi ya kipindi cha ukoloni wa kiarabu tofauti kati ya kizazi kimoja na kingine.

(vii) Mwanga na msaada wake katika kuonesha ngonjera

– Mwanga husaidia kuunganisha pamoja mambo yote yanoonekana jukwaani. Pia husaidia kuonyesha nguo wavaazo wahusika na vitu vyote vionekanavyo jukwaani na hata wahusika kuweza kuwaona waangaliaji wake.

– Na mwanga unaweza kuwa mwanga wa jua, mwezi, moto, taa za umeme, kibatari n.k.

– Hata hivyo mambo yote haya hutegemea na dhamira hiyo, ngonjera waonyeshaji na hata mavazi ya wahusika.

– Na pia katika ngonjera huweza kuambatana na muziki au ngoma hutegemea na ngonjera hiyo.

– Hali kadhalika muda mwingine huweza kuambatana na nyimbo fupi ambayo itasaidia kuonesha hali ya mchezo kwa ujumla, dhamira kusisimua n.k.

– Na muda mwingine nyimbo inaweza kufuata mwisho wa ngonjera

Tofauti Ya Mashairi Na Ngonjera

S/N Mashairi Ngonjera

Shairi huweza kutungwa ili liimbwe Ngonjera hukaririwa kwa maneno yenye kama vile redioni au lisomwe. kuonesha hali ya mazingira

Continue Studying Form Two

Get the Complete PDF Notes

Would you like these notes in a well-formatted PDF for easier reading and offline study? Click below to ask for the complete PDF notes.

GET WELL-FORMATTED PDF NOTES

View More Secondary School Notes

banner
Scroll to Top