Kiswahili Form Two Notes – Uhifadhi wa Kazi za Fasihi Simulizi

Maelezo haya ya Kiswahili Form Two yanahusu Uhifadhi wa Kazi za Fasihi Simulizi. Yamepangwa katika sehemu zilizo wazi ili kurahisisha kusoma, kuelewa na kufanya marudio.

li kitu kidumu ni lazima kihifadhiwe; fasihi simulizi kama sanaa kutokana na umuhimu wake katika jamii nayo huhufadhiwa kwa ajili ya faida ya kizazi kijacho. Katika mada hii utaweza kujifunza umuhimu wa fasihi simulizi katika jamii. Utajifunza njia mbalimbali zitumikazo katika

uhifadhi wa fasihi simulizi pia utaweza kubainisha ubora na udhaifu wa kila njia.

Njia za kuhifadhi Fasihi Simulizi

Kuhifadhi Fasihi Simulizi Bainisha njia za kuhifadhi fasihi simulizi

Umuhimu wa kazi za fasihi simulizi

Ingawa kila utanzu wa fasihi una umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zake zote zina umuhimu mkubwa katika jamii.

Kwaza fasihi hutumika kama chombo cha kuwaelimisha watu. Kupitia fasihi andishi na fasihi simulizi, watu hupata maarifa ya kutambua mambo maovu na namna ya kuyakwepa. Licha ya haya, wanajamii hujifunza njia za kujitawala, kuzalisha mali na kuishi kwa misingi ya haki, usawa na demokrasia.

Pili, fasihi ni nyenzo ya kutoa mafunzo kuhusu mambo kama vile historia, dini, siasa, jiografia na tiba. Kwa hiyo watu hujifahamisha juu ya maumbile na asili yake, mazingira, utawala, uchumi, sheria n.k.

Aidha fasihi huwapa watu mazoczi na kuimarisha uwezo wao wa kuzungumza kwa ufasaha, kuimba nyimbo kwa ufundi, kuigiza mambo kwa ustadi, kucheza ngoma kwa umahiri, kughani mashairi kwa mvuto na kusimulia matukio kwa mtindo ufaao.

Fasihi hufahamisha, huhifadhi na hurithisha mambo kuhusu utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mambo hayo ni pamoja na mila, desturi, falsafa, imani na itikadi. Pia hudumisha maarifa ya kijadi kama vile tiba, sayansi ya kilimo, uhifadhi wa mazingira na sayansi ya utabiri wa hali ya hewa.

Umuhimu mwingine wa fasihi unatokana na kutumika kwake kama chombo cha kuburudisha na

kupumbaza. Watu wanaposoma kazi mbalimbali za fasihi hupata, msisimko wa kimwili na kiakili. Kadhalika fasihi hugusa hisia za watu na kuwafanya wafurahi au wahuzunike.

Istoshe fasihi hudumisha na kukuza lugha. Watu hupanua msamiati wao na miundo ya lugha kupitia kazi zake. Hivyo fasihi inakuwa kama hazina ya maneno na dafina ya kanuni za kisarufi. Kutokana na umuhimu huu ndio maana fasihi huhifadhiwa ili isipotee. Na uhifadhi huu hufanyika kwa njia mabalimbali.

Ubora na Udhaifu wa kila Njia ya Kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi

Elezea ubora na udhaifu wa kila njia ya kuhifadhi kazi za fasihi simulizi

Fasihi simulizi inaweza kuhifadhiwa kwa njia zifuatazo:

Kichwani

Hii ndio njia ambayo imekuwa ikitumiwa kuhifadhi kazi za fasihi tangu kale na inaendelea kutumika hadi leo. Kwa kutumia njia hii kazi ya msanii hukaa kwenye ubongo wa msanii, naye huweza kuiwasilisha kazi hiyo, wakati wowote bila gharama yoyote.

Ubora wake

Uwasilishaji wa kazi hiyo unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji kufanyika maandalizi yoyote, hususani ya kiufundi.

Hakuna gharama yoyote wakati wa uwasilishaji wa kazi ya fashi. Msanii hahitaji kugharimia kitu chochote ili waweze kuitoa kichwani, ni uamzi wake tu, anaweza kuimba papo kwa papo.

Kazi ya fasihi iliyohifadhiwa kichwani ni hai. Hii ni kwa sababu msanii anakuwa ana kwa ana na hadhira yake. Kutokana na matumizi ya mbinu tofauti za kisanaa kama vile kucheza, kubadili sauti, miondoko na mengineyo mengi, kazi yake inapata uhalisia zaidi mbele ya hadhira.

Udhaifu wake

Uwezekano wa kazi kupotea au kuharibika hasa katika fani ni mkubwa. Kwa mfano msanii anapokuwa amefariki dunia kazi anayokuwa ameihifadhi kichwani nayo hupotea. Ndio maana katika baadhi ya jamii kazi za kifasihi zimepotea. Hii ni kwa sababu wasanii wanapoondoka duniani hondoka na fani hizo.

Kazi inapohifadhiwa kichwani ni rahisi kubadilika. Hii inatokea pale ambapo msanii anasahau baadhi ya maneno kutokana na umri wake au sababu nyinginezo

Njia ya maandishi

Maandishi ni njia moja wapo inayotumika kuhifadhia kazi za fasihi. Njia hii imeanza kutumika baada ya watu kujua kusoma na kuandika. Uhifadhi wa kazi za fasihi kwa njia hii hupitia njia mbili kubwa. Hatua ya kwanza ni kubuni kisa au wazo; na hatua ya pili ni kuliweka wazo hilo katika maandishi. Kazi za fasihi simulizi zinazoweza kuhifadhiwa katika maandishi ni hadithi, nyimbo, mashairi, ngonjera, majigambo n.k

Ubora wake

Kazi iliyohifadhiwa inaweza kudumu kwa muda mrefu

Kazi iliyohifadhiwa inaweza kufikia hadhira hata ya mbali na aliko msanii.

Kazi iliyohifadhiwa katika maandshi haipotezi fani yake na maudhui yake bali huendelea kuwa

katika asili yake ya awali hadi msanii atakapoamua kuibadilisha.

Udhaifu wake

— eee

ii njia ni kwa ajili ya watu wachache tu wanaojua kusoma na kuandika. Wasanii wanaoweza kutumia njia hii ni wale tu wanaojua kusoma na kuandika.

Ni aghali sana kuhifadhi kazi za kifasihi kwa njia ya maandishi. Msanii atalazimika kununua

vifaa vinavyohitajika katika maandishi ambavyo ni kalamu, karatasi, meza. Kwa hiyo ni aghali. Uwasilishaji wake si hai kwani hakuna kuonana ana kwa ana kati ya hadhira na fanani. Kwa hiyo msomaji hawezi pata vionjo vya msanii hivyo itambidi ajibunie yeye mwenyewe.

Wahusika pia hawawezi kuonekana, endapo ni igizo mabalo limehifadhiwa katika maandishi, hivyo ubora wa kazi ya msanii huchujuka.

Njia ya vinasasauti

Vinasasauti ni miongoni mwa vyombo vinavyotumika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi. Hii ni

njia iliyoendelea kuliko ile ya maandishi.

Ubora wake

Kazi ya msanii huweza kuwafikia watu hata walio mbali na alipo mtunzi.

Ikihifadhiwa katika vinasasauti kama vile tepurekoda au CD ubora wake huwa haupotei wala kuharibika endapo vifaa hivyo vitatunzwa vizuri.

Sauti ya mtunzi unaiskia moja kwa moja

Unaweza kusikia vionjo vya msanii

Udhaifu wake

Niia hii ni aghali kutumia, kununua vinasasauti ni gharama.

Uwasilishaji wake si hai, ingawa unaweza sikia sauti ya msanii au wahusika lakini hahawezi kuonekana.

Kazi yoyote ya kifasihi inapohifadhiwa katika vinasasauti, kwa mfano nyimbo, huwa ni mali ya msanii husika, mtu yeyote haruhusiwi kuitumia kama mali yake binafsi bila kuruhusiwa na msanii.

Njia ya kompyuta

Njia hii imeanza kutumika katika miaka ya hivi karibuni baada ya watu kuanza kujua na mna ya kutumia kompyuta.

Ubora wake

Njia hii ni ya uhakika zaidi kwa vile shuguli za kisanaa zinazohusika huhifadhiwa katika

kompyuta na hutolewa pale zinapokuwa zinahitajika.

Udhaifu

Msanii au wasanii wanohusika hawawasiliani na hadhira papo kwa papo. Hivyo hadhira hukosa

kuuliza maswali katika vipengele vinavyotatiza. Ili kuhifadhi kazi ya fasihi kwa kutumia njia hii ni sharti msanii awe anajua kutumia kompyuta. Pia ni aghali sana, kuzingatia kwamba kununua komputa ni gharama kubwa.

Njia ya kanda za video Msanii huweza kutumia kanda ya video kuhifadhi kazi yake. Ubora wake

Kwanza wasnii na vifaa wanavyotumia huonekana

Sauti zao na milio ya ala wanazotumia husikika na pia huonekana kwa hadhira. Hii angalau

huipa uhai kazi ya msanii mbele ya hadhira.

Huweza kudumu kwa muda mrefu endapo kanda ya video iliyotumika kuhifadhi kazi ya msanii

itatunzwa vizuri.

Udhaifu wake

Uhifadhi wa njia hii ni aghali, msanii atahitajika kununua, kanda ya video, kumlipa mpiga picha na mzalishaji pia.

Watu wanoweza kunufaika na njia hii ni wacheche mno na wengi wao ni wale wenye uwezo wa kumiliki televisheni ambao kimsingi hupatikana maeneo ya mijini.

Ingawaje hadhira wanaweza kumwona msanii lakini hawawezi kuwasiliana nae ana kwa ana,

hivyo kukosa kuuliza swali pindi wanapohitaji kufanya hivyo.

Umuhimu wa kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi

Faida ya Kuhifadhi Fasihi Simulizi

Elezea faida ya kuhifadhi fasihi simulizi

Njia zote za uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi zina umuhimu mkubwa katika ukuzaji na uendelezaji wa utamaduni katika jamii. Kama ambavyo tumekwishaona, kazi za fasihi simulizi huelimisha, huburudisha, hurithisha maarifa, maadili, pia ni vielelezo vya utamaduni wetu wa asiili. Kwa ajili hiyo ni muhimu kuzihifadhi kazi hizo zisiharibike wala kupotea ili ziendelee kutumika kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Ni muhimu ziendelee kuwepo ili kuhifadhi utamaduni wetu na huku vikitumika kama vivutio vya watalii.

Kazi za fasihi simulizi kwa upande mwingine ni sehemu ya ajira. Kwa mfano, shughuli mabalimbali za kisanaa kama vile ngoma, maigizo na utunzi wa vitabu, vinawapatia vipato

baadhi ya wasanii. Hivyo ni muhimu zihifadhiwe.

[ Kazi za fasihi simulizi pia ni kichocheo cha umoja na maclewano miongoni mwa jamii. Yote

| hayo kwa ujumla wake yanabainisha kuwepo na haja ya kuendelea kuzikusanya, kuzifanyia kazi,

kuziendeleza, na kuzihifadhi kazi za fasihi simulizi.

Maelezo Ya Ziada

Mfano: –

– Inachurura inaganda (Asali/ gundi)

– Gari la kila mtu (kifo, jeneza, miguu)

– Hamwogopi mfalme wala bawabu (njaa/ shida/ kifo)

UHIFADHI WA KAZI ZA KIFASIHI SIMULIZI

Kazi za fasihi simulizi huweza kukusanywa kwa kusikiliza wasanii wakizisimulia, kuzitamba kazi hizo mfano mkusanyaji anaweza kujiunga na wachezaji hao ambao huwa wanapiga soga na kusimulia hadithi mbalimbali. Hivyo msikilizaji anaweza kuziandika au kuzihifadhi kwa njia bora na ya kudumu zaidi.

Kuwatembelea wazee ambao ni mashuhuri katika kutamba hadithi, kughani mashairi au kutumia misemo na methali ili kuwasikiliza na baadae kuzikusanya kazi hizo tayari kwa kuzihifadhi.

Kuwasikiliza wasanii wakisimulia na kuzitamba kazi zao hivyo fanani anaweza akasikiliza, akaziandika au akazirekodi tayari kwa kuzihifadhi kwenye kichwa, kinasa sauti, filamu au maandishi.

Kuna njia mbalimbali zinazotumika katika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi.

Kichwa

Maandishi

Kanda za sauti (tepurekoda) kanda za kunasia sauti

Kanda za video, televisheni na filamu za sinema.

Kichwa

Tangu zamani uhifadhi wa fasihi simulizi upo katika kichwa cha fanani na kutolewa kwa masimulizi. Jambo hili limekuwa likifanyika kwa muda mrefu sasa, kutokana na kuhifadhiwa kichwani ndio maana fasihi simulizi ilikuwa ikirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

Bado fasihi simulizi inapohifadhiwa kichwani huendelea kuwa hai kwani hadhira na fanani huwasiliana ana kwa ana.

Hadhira huweza kumpongeza au kumhoji fanani papo kwa papo.

Fasihi simulizi kuhifadhiwa kichwani husababisha matatizo ya kupoteza kumbukumbu kutokana na kumbukumbu za akilini kufifia au kupotea hali hii ikitokea simulizi hiyo hupotea kabisa.

Kubadilisha mambo muhimu katika simulizi

Fasihi simulizi hupoteza kiini chake au ukweli wake pindi tu msimuliaji apotezapo kumbukumbu ya anayosimulia

(fanani akifa / akirukwa na akili)

Uhifadhi Katika Maandishi

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasihi simulizi inahifadhiwa katika maandishi kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye.

Kazi ya fasihi simulizi ikihifadhiwa katika njia hii haipotei au haibadiliki. Ni njia yakutunza kumbukumbu ya kudumu

– Katika maandishi fasihi simulizi haina sauti hivyo msomaji atie sauti au madaha yote mwenyewe. Hali hii inaweza kusababisha au kufikisha ubora wa kazi hiyo.

– Pia katika maandishi wahusika hawaonekani kwahiyo hadhira hushiriki kwa kuona maandishi

– Vilevile fasihi simulizi hupungua uhasilia kwani si hai tena uhai wa fasihi simulizi hujikita katika utendo na ushiriki wa fanani na hadhira.

– Huwa mali ya wachache

Fasihi simulizi tangu mwanzo ilikuwa inamilikiwa na jamii nzima kwa kuweka katika maandashi inakuwa ni mali yamsanii na hadhira yake inakuwa finyu. Hii ni kutokana na kwamba lazima ujue kusoma na kuandika ili uweze kujua kazi ya fasihi ilivyoandikwa.

– Haibadiliki kulingana na wakati na mazingira. Toka mwanzo fasihi simulizi ilikuwa ikibadilika kutokana na mazingira kwa hiyo ikibadilika mazingira nayo hubadilika na mambo yaliyosimuliwa.

– Ina gharama kwani waandishi hununua kalamu na karatasi pamoja na zana mbalimbali ili kuweza kutoa kitabu.

Uhifadhi Wa Vinasa Sauti

Hizi ni zana zitumikazo kurekodi sauti mfano; tepurekodi,kanda za muziki na sauti CD n.k

– Katika njia hii ukweli wa sanaa ya kazi haitabadilika. Sauti ya wahusika halisia itaendelea kusikika kama ilivyotolewa hivyo fasihi simulizi haipotei wala kubadilika badilika.

– Njia hii inatunza kumbukumbu.

– Utendaji wa wahusika hawaonekani kwahiyo hadhira itashiriki kwa kusikiliza kanda kwahiyo sio hai.

– Haitabadilika kulingana na mazingira na wakati. Kubadilika kwa mazingira hubadilisha mambo yanayosimuliwa lakini fasihi simulizi iliyorekodiwa kwenye vinasa sauti ikisharekodiwa haibadiliki. Hivyo kutaendelea na mabadiliko ya nyakati na hali halisi ya wakati huo

– Ni ghali mno. Fasihi simulizi iliyorekodiwa katika kanda ni ghali mno kiasi kwamba huwa shida kwa hadhira kuipata na pia kuirekodi huitaji pesa, hivyo ni ngumu kuhifadhi fasihi simulizi kwa njia hii.

Kanda Za Video, Runinga, Tanakilishi Na Filamu Za Sinema

Kanda za video hurekodi sauti na sura. Picha hizo huoneshwa kwenye video na runinga. Picha za sinema hupigwa kwa aina maalumu za kamera ambazo huoneshwa na projecta na huonekana watu na matendo yote yatendwayo. Hivyo kwa kutumia filamu za video tunaweza kuhifadhi na kuonesha kazi za fasihi simulizi.

– Huweza kutunza kumbukumbu za muda mrefu na zilizohifadhiwa kwa njia hii hazipotei au kusahaulika.

– Haibadiliki kutokana na mazingira na nyakati kwa kubadilika kwa mazingira hubadili usimulizi lakini njia hii haiwezi badili usimulizi pindi tu ukisharekodiwa hivyo kutoonesha uhalisia wa mazingira na nyakati.

– Ni ghali mno. Fasihi simulizi iliyorekodiwa katika filamu au redio huwa aghali mno wakati wa kurekodi. Pesa nyingi huitajika ili uweze kurekodiwa na vifaa vitumikavyo ni aghali sana na hata ikisharekodiwa bado huuzwa aghali ili uweze kurudisha gharama zilizotumika katika kurekodi, hivyo huwafikia wale tu wenye uwezo wa kifedha. Hivyo si mali ya jamii nzima.

– Kwa kuwa fasihi simulizi imejikita kwenye shughuli na tabia za kila siku za jamii ni wazi kuwa fasihi simulizi ni hai. Kwa hiyo ni vyema tukahifadhi fasihi simulizi za kale na sanaa.

– Lengo kuu la kuhifadhi fasihi simulizi na kale ni sisi kuzifanya zisipotee.

– Pia ili tuweze kutumia mali za jamii yetu kwa kuwa kuhifadhi nyimbo ni kazi nyingine za kisanaa ni tuzo na kumbukumbu tosha kwa vizazi vijavyo.

Continue Studying Form Two

Get the Complete PDF Notes

Would you like these notes in a well-formatted PDF for easier reading and offline study? Click below to ask for the complete PDF notes.

GET WELL-FORMATTED PDF NOTES

View More Secondary School Notes

banner
Scroll to Top