Kiswahili Form One Notes – Usimulizi

Kiswahili Form One Notes – Usimulizi

Full text version of Kiswahili Form One Notes on Usimulizi, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.

Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 23-24. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cho kwanza

MADA YA TANO: USIMULIZI

Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Katika
‘mada hii utajifunza juu ya taratibu za usimulizi wa matukio kupitia njia kuu mbili za masimulizi,
yaani kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi. Pia utaweza kujifunza juu ya mbinu
mbalimbali za usimulizi
Usimulizi wa Hadithi
Usimulizi hufanyika kwa njia kuu mbili yaani kwa njia ya maandishi na kwa njia ya masimulizi
ya mdomo. Kila njia hutegemea namna msimuliaji anavyoweza kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa
msimuliaji na msikilizaji hawakukaribiana, njia ambayo itatumika ni ile ya maandishi. Kwa
mfano kama utahitaji kumweleza mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika
kutumia maandishi, yaani utatumia njia ya kumwandikia barua. Lakini kama unamsimulia mtu
ambaye yupo karibu nawe, utatumia njia ya mazungumzo ya ana kwa ana.
Jsimulizi wa Habari
Taratibu za Usimulizi wa Matukio
Usimulizi wa matukio dhamira yake ni kumweleza mtu au watu tukio ambalo wao
hawakulishuhudia. Hivyo katika usimulizi msimuliaji hutakiwa kutoa maclezo muhimu ambayo
yatawawezesha watu hao kulielewa tukio linalosimuliwa sawasawa na huyo anayeshuhudia.
Mambo muhimu ya kutaja katika usimulizi wa matukio ni pamoja na haya yafuatayo:
1. Aina ya tukio~ msimuliaji atatakiwa kubainisha katika maclezo yake aina ya tukio. Kwa
‘mfano, kama ni harusi, ubatizo, ajali ya barabarani au mkutano.
2. Mahali pa tukio — ili msimuliaji aweze kuielewa habari inayosimuliwa, ni lazima
Kumwelewesha ni mahali gani tukio hilo limetokea. Kwa mfano, kama ni mjini inafaa
‘kutaja hata jina la mtaa.
3. Wakati —katika usimulizi ni muhimu pia kutaja muda ambao tukio limetendeka kama ni
asubuhi, mchana au jioni bila kusahau kutaja muda halisi yaaniilikuwa saa ngapi.
4. Wahusika wa tukio — ni muhimu kutaja tukio limehusisha watu gani, wingi wao, jinsia
‘yao, umri wao nk
5. Chanzo cha tukio — kila tukio lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa katika
usimalizi
6. Athari za tukio — athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Kama ni ajali, je watu
‘wangapi wameumia; wangapi wamepoteza maisha n.k.
7. Hatima ya tukio ~ msimuliaji katika usimulizi wake ni lazima abainishe baada ya tukio
kkutokea na kushughulikiwa hatima yake ilikuwaje. Kwa mfano, kama tukio ni ajali ya
barabarani hatima yake inaweza kuwa majeruhi kupelekwa hospitalini na dereva
aliychusika kukamatwa.
Kwa hiyo misingi hii ya usimulizi hufanya usimulizi wa tukio kuwa na schemu kuu tatu:
‘+ Utangulizi — sehemu hii huwa na maclezo tu ya utangulizi ambayo hulenga kuvuta hisia
na umakini wa msikilizaji au wasikilizaji. Kwa kawaida utangulizi wa tukio huwa ni
maneno machache kiasi yasiyozidi aya moja.
‘+ Kiini —kiini cha usimulizi huelezea tukio halisi kuanzia chanzo chake, wahusika, muda,
‘mahali na athari za tukio,
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
‘+ Mwisho — mwisho wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya mwisho ya tukio
linalohusika, wakati mwingine matukio haya yanaweza kuambatana na maclezo ya
‘msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio ambalo amesimulia.
Mbinu za usimulizi
Ti habari inayosimuliwa ipate kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za kusimulia
katika hali inayovuta hisia za msikilizaji wake
Baadhi ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi sahihi ya
Kiswahili
Kwa upande wa uigizi msimuliaji atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio
ambalo anasimulia, Nayo ni kama vile milio, sauti na matendo,
Kwa upande wa usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti usimulizi huo uwe na
kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa kwa maneno yasiyovidi matano,
yaliyoandikwa kwa herufi kubwa,
Kwa vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa katika
wakati uliopita.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————

GET ORIGINAL PDF NOTES THROUGH 255620339260

banner
Scroll to Top