Kiswahili Form One Notes – Uandishi wa Insha

Kiswahili Form One Notes – Uandishi wa Insha

Full text version of Kiswahili Form One Notes on Uandishi wa Insha, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.

Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 25-26. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cho kwanza

MADA YA SITA: UANDISHI WA INSHA

Uandishi Wa Insha

Uandishi ni kitendo cha kupangilia maneno katika maandishi. Mada hii inazungumzia uandishi
wa insha za wasifu kwa umahususi wake. Kabla ya kuanza uandishi utajifunza mambo muhimu
‘yanayopaswa kuzingatiwa katika uandishi wa insha kwa ujumla. Utaclewa mundo wa insha na
‘mwisho utajifunza juu ya dhana ya insha ya wasifu na namna inavyoandikwa na mwisho kabisa
uutaangalia mfano wa insha ya wasifu
Insha za Wasifu
Insha ya wasifu ni ile ya kutoa maclezo juu ya jinsi mtu au kitu kilivyo, tabia, vitendo na
mandhari (sura ya mahali jinsi panavyoonekana).
Mambo muhimu katika insha ya wasifi ni: sura, rangi, umbo, vipimo, tabia, na kadhalika. Insha
hizi zinaweza kuongelea kitu chochote kile, inaweza kuwa ni mnyama, mtu, Shule, nchi na
kadhalika.

Hatua za Uandishi wa Insha

Kabla ya kuanza kuandika insha, ni muhimu sana uamue unataka kuandika juu ya nini. Inafaa
uuchague ile mada iliyo rahisi kwako kuweza kujieleza kikamilifu na kwa urahisi.
Kama unaandika insha za kufanyia mazoezi ni heri uchague mada zenye habari ambazo
unazielewa. Iwapo hulijui au hulielewi jambo, ufanye uchunguzi kwanza. Ukisha kupata habari
muhimu ndipo baadaye uandike insha yako kulingana na jinsi unavyoijua na jinsi
unavyoikumbuka habari inayohusika.
Katika mtihani ni muhimu uyasome maagizo kwa makini. Kwa mfano, maagizo yanaweza kuwa:
Chagua mojawapo ya habari zifuatazo kisha uandike insha isiyopungua kurasa mbili za karatasi
za majibu.
Au:
Chagua mojawapo ya habari hizi kisha uandike insha ya maneno yasiyopungua 400.
Ni heri uandike insha nzuri ya kiwango kinachotakiwa kuliko ndefu (zaidi ya maneno 400)
ambayo haitakuwa na mambo muhimu hadi mwisho, na pengine yenye makosa na uchafu
mwingi kupindukia. Ni muhimu ikumbukwe jinsi insha ilivyo ndefu, hasa katika mtihani, ndivyo
idadi ya makosa inavyozidi kuongezeka.
Muundo wa Insha
Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:
1. Kichwa cha insha; kichwa’cha insha hudokéza kile ulichokijadili katika insha yako.
Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k
2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili_ ya maneno
‘muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili Katika insha
yako.
3. Kiini cha insha; katika kiini ndipo kuna maclezo ya kina jum ya kile unachokijadili
kkatika insha yako, maclezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja
ulizonazo katika mjadala wako.
4. Hitimisho; hapa ndipo kuna mubtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au
inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Hebu soma mfano ufuatao wa insha ya wasiu:
Mfano 1

SHULE YANGU

Shule yangu inaitwa Shule ya Sekondari ya Mwananchi. Ni shule ya zamani
iliyoanzishwa siku ya [umaa, tarche 5 Agosti 1966 na Mheshimiwa Donna Matembele,
aliyekuwa diwani wa kata ya Masuba.
Shule hii ambayo ni maarufu sana ipo katika Tarafa ya Mkunazini. Imejengwa katika
uwanja wa hekta kumi na mbili. Ina madarasa kumi na mawili ya vidato vinne vya mikondo
mitatu kila kimoja. Ina wanafunzi mia tano na wanne badala ya idadi halali ya wanafunzi mia
inne themanini. Ni shule inayopendwa sana.
‘Wanafunzi wa kike ni mia mbili na watatwina Wa kiume ni mia’tatu na mmoja. Walimu ni
thelathini na mmoja. Jamii hii inapendana sana. Wanafunzi wana imani kubwa sana na walimu
wao. Walimu huwahimiza wawe wanafanya bidii katika kazi na masomo kwa yjumla.
Wanafuunzi hukadiria ugumu wa mazoezi wapewayo. Yale wayaonayo kuwa ni rahisi wao
hujifanyia. Yale magumu kidogo hushughulikia kwa pamoja kwa kusaidiana wenyewe kwa
wenyewe, Walimu hushirikishwa tu wakati wa mazoezi tata,
Shule ya Sekondari ya Mwananchi ni ya kuvutia sana. Ina miti mingi sana ya matunda,
Ina maua ya aina aina, Kutokana na nidhamu na uwajibikaji matunda hukomaa ndipo yatumiwe
kwa mpango wakati wa chakula,
Heshima imethaminiwa mno na wanafunzi. Wanaheshimiana na kuwaheshimu walimu wao.
Kwao heshima ni utiifu na uzingativu. Kutii na kuzingatia mambo waambiwayo na walimu
ndicho kipimo cha heshima.
Katika shule yangu wanafunzi tuko kama paka. Paka hamtumi mtu nyama lakini
atunukiwapo kipande hawezi kumruhusu yeyote kukigusa.Nasi tutunukiwapo nafasi yoyote ya
kusoma hatumruhusu mtu yeyote kutupokonya nafasi hiyo.
Wanafunzi wa shule wana sare zao za kuvutia wazivaazo kiungwana kabisa. Sare hizo ni sweta
ya bluu, shati au blauzi ya samawati, tai ya rangi ya damu ya mzee, suruali ndefuu au sketi ya
ikijani kibichi, viatu vyeusi vya soli ndogo na visigino vifupi.
Katika shule yetu kuna uhusianao mwema baina ya walimu, wazazi, Chama cha Wazazi
na Walimu (CHAWAWA) na Baraza la Shule. Kamati ya CHAWAWA na Baraza la Shule
huanzisha miradi na kuitekeleza haraka kutokana na wazazi kuiunga mkono.
Kwa muda mrefu sasa matokeo ya mitihani yamekuwa ya kuridhisha kabisa.Na si hayo peke
yake. Wanafuunzi washirikipo katika michezo ya mpira, ya riadha na matamasha ya muziki
takribani mara zote huibuka washindi.
Kwa ufupi shule yangu ni ya mafanikio meng.
Mambo muhimu ya kuzingtiwa katika insha hii ya wasifu:
+ KICHWA (Shule yangu),
+ MAELEZO KAMILI yenye:
+ JINA la shule
+ HISTORIA ya shule
+ MAZINGIRA ya shule
+ IDADI ya wanafunzi na walimu
+ HALT ya wanafunzi
+ MAFANIKIO ya shule.
+ HITIMISHO lenye sifa ya jumla.
Insha za Kisanaa na zisizo za Kisanaa
Tofautisha insha za kisanaa na zisizo za kisanaa
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————

GET ORIGINAL PDF NOTES THROUGH 255620339260

banner
Scroll to Top