Kiswahili Form One Notes – Uandishi wa Barua

Kiswahili Form One Notes – Uandishi wa Barua

Full text version of Kiswahili Form One Notes on Uandishi wa Barua, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.

Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 27-28. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Zoezi 1 Tofautisha insha za kisanaa na zisizo za kisanaa,

MADA YA SABA: UANDISHI WA BARUA

Uandishi Wa Barua

Barua za kirafiki ambazo pia huitwa za kindugu huandikwa baina ya watu wa undugu au jamii
moja. Katika mada hii utaweza kujifunza muundo, wa uandishi wa barua ya kirafiki na jinsi ya
kuandika barua ya kirafiki, Utaweza kutofautisha kati ya barua ya kirafiki na ile isiyokuwa ya
kirafiki.
Barua za Kirafiki
Iwapo ni katika ndugu barua za kirafiki zaweza kuwa kwa watu kama: baba, mama, shangazi,
mume, mke, mtoto, na kadhalika. Katika jamii waandikiwao barua za kirafiki ni kama jirani,
rafiki, mpenzi, mwalimu, mwanafuunzi, daktari, mgonjwa, na kadhalika
Muundo wa Barua za Kirafiki
Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa barua za kirafik:
+ ANWANI kamili ya mwandishi, katika herufi hukaa juu upande wa kulia mwa karatasi.
+ TAREHE, chini ya anwani.
‘+ MTAJO wa heshima kwa anayeandikiwa, kama vile, mpendwa, mpenzi, na kadhalika,
hhuandikwa kushoto, baada ya tarehe.
‘+ UTANGULIZI wa barua yenyewe ambao kwa desturi huwa ni salamu.
+ BARUA YENYEWE ambayo ndiyo kiini cha waraka.
+ SALAMU za kumalizia, pengine kwa jamaa na jamii
+ HITIMISHO, katika aya, maalumu ambayo huwa, kwa mfano: ‘Ni mimi baba yako
akupendaye,” na kadhalika
‘+ SAHIHI ambayo si sharti wala muhimu sana,
+ JINA au MAJINA ya mwandishi, mwishoni
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
‘Tazama mfano wa barua ya kirafiki:
Mfano 1

MUSOMA FISH PACK

S.LP 4546

MUSOMA,

23/5/2018
Mwanangu Nyamchele,
‘Ninafuraha kukujulisha kuwa nimepokea barua yako. Mambo yote uliyoyacleza
nimeyaelewa barabara, HukU nyuimbani sote tu wazima nani matumaini yetu kwamba afya yako
ni nzuri.
Tabia ya kulalamikia chakula ni mbaya. Tabia kama hii ikikomaa husababisha ulafi. Kumbuka
hukwenda shuleni kula kama nguruwe, Huko shuleni:nimekupeleka ili usome kwa bidii na
Ujifunze mengi. Usitamani kustarehe na kufikiria maakuli na anasa zingine za ulimwengu huu.
Ondoa fikira za chakula akilini mwako na uache uzembe, eboo!
Hebu nikuonye kubusu. kuwapima na kuwachagua walimu. Walimu katika shule hiyo ni
wabobezi na ndio maana nikakupeleka hapo. Wanajua mnayostahili kufundishwa, Huna ruhusa
ya kusema eti walimu wengine ni wakali na hufundisha haraka haraka sana. Wewe unahitaji
ikutega sikio na kuti. Ukiwa makini na uwe na imani utayaclewa mambo unayofundishwa,
Usisahau kuwa mchagua jembe si mkulima.
Mambo makubwa unayostahili kuyatilia bidii ni masomo yako. Muda wa miaka minne ni
mfupi sana. Uonyeshe adabu njema kila wakati. Uwaonyeshe walimu wako taadhima na uwatii
daima dawamu.
Jambo lililo kubwa katika shughuli yoyote ni uvumilivu. Ukivumilia utavuna matunda
mabivuSitachoka kukusisitizia, ‘Ukilima pantosha, utavuna pankwisha.’ Fanya kila jitihada
utimize mambo mengi iwezekanavyo kuanzia leo lakini usipapie chochote. Ndo ndo ndo hujaza
ndoo.
Mungu akubariki.Umwombe akusaidie katika kila jambo. Ujiepushe na maovu yoyote
yale. Ukiwa na jambo usiwe na hofu kutuarifu mara moja. Mama yako amekusalimu sana.
‘Amenikumbusha nikupashe hakuna refi lisilo na ncha.
Kwaheri kwa sasa
Ni mimi, baba yako akupendaye,
Magafu: Malima
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————

GET ORIGINAL PDF NOTES THROUGH 255620339260

banner
Scroll to Top