Kiswahili Form One Notes – Mawasiliano
Full text version of Kiswahili Form One Notes on Mawasiliano, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.
Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 2-6. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cho kwanza
MADA YA KWANZA: MAWASILIANO
Katika mada hii unatarajiwa kuelewa fasili ya mawasiliano na jinsi mchakato wa mawasiliano
unavyofanyika. Utaelewa dhana ya lugha na vipengele muhimu vinavyokamilisha fasili ya lugha.
Utaelewa dhima kuu za lugha, matumizi na umuhimu wake. Vilevile katika mada hii utajifunza
jjuu ya lafudhi na matamshi mbalimbali ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili
Lugha kama Chombo cha Mawasiliano
Mawasiliano ni mchakato wa kuhawilisha taarifa kwa njia ya ubadilishanaji wa mawazo, hisia,
malengo, tabia, matarajio; ‘mitazamo¥ kupitiay mazungumzo, sishara na maandishi. Ni
ubadilishanaji wa taarifa unaoleta maana baina ya pande mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa
viumbe hai au kinyume chake. Sasa hapa sisi tutajikita katika mawasiliano yanayofanywa baina
ya viumbe wanaotumia lugha (ambao kimsingi ni binadamu)..
Maana ya Mawasiliano
Lugha ni nyenzo muhimu sana katika mawasiliano ya binadamu. Ulishawahi kujiuliza kwamba
muwasiliano yangekuwaje pasipokuwepo lugha?Mwalimu angekua anatumia mtindo gani
kukufundisha darasani au wewe ungemwombaje kalamu rafiki yako? (Unasema ungewasiliana
kama wanavyowsiliana watu wasiosikia au kuzungumza?) Hao pia wanawasiliana hivyo kwa
sababu wana maarifa ya lugha
Mafumbuzi ya kisayansi na teknolojia, yote haya yasingewezekana pasipo kutumia lugha,
uusingeweza kusogoa (kuchat) na marafiki zako kwenye facebook, usingeweza kumwandikia
tujumbe rafiki yako kupitia simu yako na kadhalika.
Umeona sasa jinsi lugha ilivyo muhimu katika mwasiliano?Kabla hatujaona umuhimu huu hebu
tuangalie fasili/maana ya lugha.
Kuna mitazamo mbalimbali juu ya fasili ya lugha lakini kwa ujumla lugha inaweza kufasiliwa
kama mfumo wa sauti za nasibu zilizokubaliwa na watu au jamii ili zitumike katika
‘mawasiliano yao ya kila siku ili kuelezea hisia, mawazo, matakwa na mahitaji yao.
Kulingana na fasili hii tunaweza kubainisha maneno ya msingi yanayojitokeza katika fasili ya
lugha, maneno hayo ni pamoja na haya yafuatayo:
Lugha ni mfumo.
Kila lugha ya mwanadamu imeundwa katika mifumo miwili mikuu; mfumo wa sauti na mfumo
wa maana. Lugha huundwa kwa sauti ambazo huunganishwa kuunda neno au sehemu ya neno,
maneno nayo huungana kuunda miundo mikubwa zaidi yenye maana kama virai, vishazi,
sentensi na aya. Mfano; k+u+k+u — kuku
Mtoto + anatembea — mtoto anatembea
Katika muunganiko huw wa maneno na miundo,mbali mbali, huwa kuna kanuni na sheria
Zinazodhibiti mfuatano wa kila kipashio. Kuna kanuni zinazodhibiti mfuatano wa sauti,
mfuatano wa mofimu, mfuafano wa maneno na hata mfuatano wa sentensi, Kwa maana hiyo,
lugha ya mwanadamu ni mfumo wenye kanuni, sheria na taratibu maalumu ambazo zikikiukwa
basi kunakuwa hakuna utimilifu wa lugha husika. Sheria hizi zinazotawala mpangilio wa viunzi
vya lugha hiyo ndizo zinazowawezesha watumiaji wa lugha fulani kuelewana.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
Kiswahili kidato cha kwanza
Lugha ni mfumo wa sauti nasibu
Lugha ni ya nasibu kwa maana kwamba, hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno (kwa mfano jiwe) na kitu chenyewe tunachotumia katika ujenzi na matumizi mengine (maana na kirejelewa). Hii ina maana kwamba, maumbo ya ishara za kiisimu hayana uhusiano wowote au mfanano wowote na maana ambazo tunayapa. Kwa mfano neno “jiwe” hakuna watu waliokaa na kusema kuanzia leo hili litaitwa jiwe. Vile vile hakuna uhusiano wowote kati ya neno “jiwe” na umbo linalorejelewa. Uhusiano wake ni wa nasibu tu na hutofautiana kutokana na lugha moja na nyingine. Jiwe mnaliitaje katika lugha yenu? Basi huo ndio unasibu wa lugha.
Lugha ni maalumu kwa mwanadamu
Lugha ni chombo cha mawasiliano ambacho amejaliwa binadamu tu na kwamba hakuna kiumbe mwingine ambaye si binadamu mwenye uwezo wa kuzungumza na kutumia lugha. Hii ina maana kuwa kuna sifa fulani za lugha za binadamu ambazo hazipatikani kwa kiumbe mwingine yeyote yule isipokuwa mwanadamu. Ingawa ndege, mbwa, nyuki, tumbili wanaweza kuwasiliana, mawasiliano yao huwa ni ya sauti au ishara ambazo kimsingi siyo lugha, pia huwa yanadhibitiwa na hisia tu kama hofu, njaa, na ishara za kutoa taarifa. Binadamu ana uwezo wa kujifunza lugha mbalimbali na kuitumia katika mazingira yake na kitu ambacho wanyama hawawezi. Kwa mfano, ukimchukua paka wa china na kumleta Tanzania atatoa sauti ile ile sawa na paka wa Tanzania kwa kueleza shida ile ile au kutoa ishara ile ile.
Lugha ni mfumo wa ishara
Uishara wa lugha unamaanisha kuwa maneno huambatanishwa/huhusishwa na vitu, matendo, mawazo au hisia kwa makubaliano ya unasibu tu. Vile vile, yale tunayoyasoma katika maandishi ni ishara tu, maana zake lazima zipatikane katika muktadha wa mawasiliano. Hivyo basi, tunapojifunza lugha lazima tufahamu mfumo wa alama za lugha hiyo na kuelewa uhusiano uliopo kati ya ishara na vitu vinavyowakilishwa.
Lugha hutumia sauti
Sifa kuu ya lugha ni kutumia sauti ambazo hutengenezwa na ala za sauti. Pamoja na maendeleo ambayo mwanadamu ameyafikia kwa sasa katika uandishi na uwasilishaji wa taarifa kwa kutumia lugha sauti ndiyo msingi wa kila kitu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba:
a. Mtoto hujifunza kuzungumza kabla hajajifunza kusoma na kuandika.
b. Mtoto hujifunza lugha moja kwa moja bila kufikiri kadiri anavyokuwa
c. Maandishi yalikuja baada ya mazungumzo
d. Maandishi huwasilisha yale yanayozungumzwa
e. Watu kwa kawaida hutumia muda mwingi kuzungumza kuliko kuandika
Kuna mambo mengi ya muhimu katika sauti za lugha ambayo hayawezi kuwasilishwa vema kwa kutumia maandishi. Mambo hayo ni kama, kiimbo, toni, mkazo, kidatu; haya ni muhimu katika mawasiliano lakini hayawezi kuwasilishwa kisawasawa kwa kutumia maandishi.
Lugha ni kwa ajili ya mawasiliano
Kwa kutumia lugha binadamu anaweza kufanya vitu ambavyo viumbe wengine hawawezi kuvifanya. Vile vile lugha hutuwezesha sisi kuzungumzia hisia zetu, matamanio yetu, kucheza, kufanya kazi n.k. Yote haya yanawezekana kwakuwa tunayo lugha ambayo ndiyo nyenzo kuu ya mawasiliano.
© tzshule 2019 | tzshule@gmail.com
Kiswohill kidato cha kwanzo
Mfumo wa Lugha
Hoja kuwa lugha ni mfumo inamaanisha kuwa lugha ina muundo unaohusisha viambajengo
‘mbalimbali. Viambajengo au vipashio hivi ni sauti,neno na sentensi. Kwa pamoja, vipashio hivi
hhushirikiana kuunda tungo zenye maana na Kama tungo hizo hazina maana au kama
haziwasilishi ujumbe wowote basi tunasema haziwi lugha.
Dhima za Lugha katika Maws
iano
FFafanua dhima za lugha katika mawasiliano
Baadhi ya dhima za lugha ni pamoja na hizi zifuatazo:
a
‘Ujumi: ujumi ni hali ya kutumia maneno ya lugha fulani kwa ufundi na ustadi wa hali ya
Jjuu kwa lengo la kuburudisha na kuwavutia watu wengine. Baadhi ya watu hutumia lugha
wa dhima hiyo, ili maksudi wasomaji au wasikilizaji
ao wavutike na kuburudishwa na
Lugha hiyo. Maeneo yatumikamo lugha yenye ujumi wa kiwango cha juu ni kwenye
matangazo na kwenye fani’ya utunzi wa mashaiti.
Utambuzi
Ni hali ya kufikiria kwa makini, kukokotoa na kutoa majibu ya maswali
tofauti ndani ya ubongo. Chombo kikuu kitumikacho kutoa majibu hayo ni lugha.
Kutokana na muktadha huo tunaweza kusema kwamba lugha hutumika kama chombo
cha wtambuzi.
Hi
ni fikra za ndani alizokuwa nazo kiumbe mwanaadamu, Tunapotaka kuonyesha
hisia zetu na vilevile kuwavuta wengine kwa maneno mazito yanayowera kumtoa
msikilizaji machozi ya huzuni au ya furaha tunachagua maneno makali yenye hisia,
Kujielezea: Hali ya mtu kudhihirisha mambo mbalimbali aliyoku
‘ayo ndani ya moyo
wake. Kwa mfano mtu anaposema nina furaha sana. Hapa mtu anatowa msisitizo wa
kuonyesha kiwango cha furaha
ichonacho, hili linafanyika kwa kutumia lugha. kwa
ufupi tunachoweza kusema hapa ni kwamba lugha hutumika kwa ajili ya kujiclezea.
Kuamuru: Ni kutoa maclekezo kwa njia ya kuamrisha. Kwa mfano hakimu
anamuhukumu mshitakiwa kwakumuamuru ‘Ninakufunga miaka mitatujela
Hapa lugha
atenda kazi ya kuaruru,
Kushirikiana: ni hali ya kutenda kitu kwa pamoja au hali_ya kuwa na ubiya kwenye
Jambo. Lugha huwezesha watu kujenga mahusiano ya siri baina ya watu wawili au zaidi
na kuweza kujitengenezea njia za0 za kuwasiliana pasipo wengine kuclewa
Kuonesha: kumuelekeza mtu kitu kwa njia ya kuashiria. Unapotaka
kuonesha jambo ni lazima utumiye lugha kwa njia moja au nyengine.
Matumizi na Umuhimu wa Lugha
Lugha hutumika kama chombo, zana, kifaa au njia ya kufikia lengo’fulani. Baadhi ya matumi:
ya lugha ni pamoja na haya yafuatayo:
Kuwasi
: Luigha hutumika kupashana habari
Kuunganisha- Lugha hupatanisha na kuleta uclewano miongoni mwa wanajamii. pia
ugha huweza|
stofautisha jamii moja na nyengine.
Kujenga jami
ugha huleta/huhimiza shughuli za maendeleo ya jamii, huleta amani na
mmshikamano katika jam
Kufundis
Lugha hutumika katika kufundishia climu,
Kutamb
isha- Lugha hutumika kutambulisha jamii ya watu fulani.
Kuhifadhi- Lugha ndicho chombo cha kuhifadhi na kueneza utamaduni
lors
Ttashele@ameil.com
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Matamshi Na Lafudhi ya Kiswahili
Matamshi ni namna ambavyo mtu anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza lugha.
Unaposema fulani ana matamshi mazuri ya Kiswahili utakuwa unamaanisha anazungumza
Kiswahili fasaha.
Neno moja linaweza kuzungumzwa/kutamkwa kwa namna tofauti na watu mbalimbali kutokana
na sababu mbali mbali, sababu hizo ni pamoja na eneo la kijiografia anakotoka huyo mtu, kabila
lake, kundi lake la kijamii mfano msanii au mwanasiasa, na elimu aliyonayo, Hizi zote zinaweza
zikawa ni sababu za kufanya watu watofautiane katika matamshi.
Dhana ya matamshi huhusisha:
‘+ Sauti za lugha husika
+ Mkazo
+ Kiimbo.
Sauti za Lugha ya Kiswahili
Sauti za lugha ya Kiswahili hujumuisha irabu na konsonanti, ambazo kwa ujumla huunda sauti
24, irabu tano na konsonanti 19 (konsonanti x na q hazipo katika matamshi ya kiswahili). Sauti
za Kiswahili hutamkwa kama zilivyoandikwa, kwa mfano maneno “data” au “dengue” wewe
uunayatamkaje? Wengi huyatamka kama yalivyo hata kama wakiwa wanazungumza kiingereza,
hii ni kwa sababu maneno ya Kiswahili hutamkwa kama yalivyoandikwa,
Kwa hiyo unapotamka maneno ya Kiswahili ni sharti uzingatie sauti asilia za lugha ya Kiswahili
Kuna watu huwa wanaandika hivi “xaxa”, hii huwa unaitamkaje?Au “ucjal” huwa unaitamkaje?
Kwa kufuuata matamshi asilia ya Kiswahili “ucjal” itatamkwa “uchijal” sijui itakuwa ina maana
gani sasa. Na pengine umekuwa ukitumia maandishi ya namna hii hata kwenye insha zako
ukidhani upo sahihi au ni kwa mazoea tu, sasa kwa kuwa umejua matamshi sabihi ya Kiswahili
ni yapi, utajifunza kuyatumia kwa usahihi katika maandishi rasmi na yasiyo rasmi
Mkazo
Katika lugha ya Kiswahili kuna namna ya kutamka maneno ili kuleta maana mbali mbali, kwa
mfano neno “barabara” litaleta maana husika kulingana na jinsi lilivyotamkwa. Hivyo, mkazo ni
pale silabi inapotamkwa kwa kukazwa. Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo
hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa mkazo, sauti
hupandishwa juu kiasi.
Maneno mengi ya Kiswahili, hasa yale yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika silabi ya pili
kutoka mwisho.
Kwa mfano:ba ‘bu, maya, rama’ni (mimi nilikuwa nikitamka ra’mani), baraba’ra (njia).Baadhi
ya maneno yenye asili ya kigeni, huwa na mkazo katika silabi nyingine. Kwa mfano: bara’bara
(awa sawa), Atha misi
Kiimbo
Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unajitokeza katika utamkaji
wa lugha fulani,
Katika utaratibu wa utamkaji, dhana ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya kidatu ( yaani ,
kiwango cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaj), Kwa hivyo ni muhimu hapa
kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu. Wakati kimbo kina maana ya kupanda na
kushuka kwa mawimbi ya sauti ya lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo,
wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Aina za viimbo
+ Kiimbo cha maclezo: Kiimbo cha maclezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji wa
ugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji wake yanakuwa
takriban katika mstari ulionyooka. Mfano, Mwalimu anafundisha,
+ Kiimbo cha maulizo: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya
kkidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa. Mfano, mwalimu anafundisha?
+ Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiani sana na kiimbo cha maulizo. Kiimbo
cha amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha ju zaidi kuliko ilivyo katika kimbo cha
maclezo. Mfano, njoo hapa!
Lafudhi ya Kiswahili
Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira.
Mazingira hayo yanaweza kuwa enco atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha
elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa watumiaji wengi wa Afrika Mashariki, kwa hiyo hii
inafanya kuwatambua wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila yao au macneo
wanakotoka. Kwa mfano, kwa hapa Tanzania tunaweza kuwatambua watu wa Mwanza kwa
lafudhi yao, watu wa Mtwara kwa lafudhi yao, watu wa Pemba kwa lafudhi yao au watu wa
Musoma kwa lafudhi yao. Mifano:
a. Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa (Wakuria)
b. Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mafaranga makumi mawili (Wakongo)
. Ukikaa nchale, ukichimama nchale (Wamakonde)
4. Wewe unakamuaga mang’ombe tu moja kwa moja (Wasukuma)
e. Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado
uunaningangania tu! (Wahaya)
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————