Kiswahili Form One Notes – Aina za Maneno
Full text version of Kiswahili Form One Notes on Aina za Maneno, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.
Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 7-15. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cho kwanza
DA YA PILI: AINA ZA MANENO
Katika lugha ya Kiswahili kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa
lugha wanakubaliana hivyo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina zote nane za
maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia kyjifunza namna ya kutofautisha aina
za maneno ambazo zimeleta ubishi miongoni mwa wataalamu wengi hususani katika
Viunganishi na Vihusishi.
Ubainishaji wa aina Saba za Maneno
‘Aina Saba za Maneno ya Kiswahili
Bainisha aina saba za maneno ya Kiswahili
Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo:
1. Nomino (N)
2. Viwakilishi (W)
3. Vitenzi (T)
4. Vivumishi (V)
5. Vielezi (E)
6. Viunganishi (U)
7. Vihusishi (H)
8. Vihisishi (I)
Ufafanuzi wa aina za Maneno
‘Nomino (N)
‘Nomino ni maneno yanayotaja vitu, watu, na hali kadhalika. Kuna aina mbali mbali za maneno
ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo:
‘+ Nomino za pekee:Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za
kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote, Hizi ni nomino
zinazobusisha majina kama vile-ya’watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari
Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata kama nomino hizi zinapatikana
katikati ya sentensi.
+ Nomino za kawaida:Hizi kwa jina jingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi
hazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu,
mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Bahati, Bite ama Neema. Ikiwa ni mlima
hautambuliwi kama ni Meru , Kilimanjaro au Evarest, yaani hutaja vitu bila kutaja
umahususi wake kama jilivyo katika nomino\ za pekee.Hizi zinapoandikwa si lazima
zianze na kwa herufi kubwa ispokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au
zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu
‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, Jakini hapa inaanza kwa herufi kubwa
‘kwani inataja anuwani ya kipckee.
+ Nomino za mguso:Nomino za mguso hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na
mwanadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi-
yaani vitu vinavyoweza kushikika, kuonekana, kunusika na kuonjeka.
+ Nomino za jamii:Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja,
‘yaani nimino zinazotaja umla ya vitu vingi. Mfano; jozi ya viatu, umati wa watu, bustani
‘ya maua, bunga ya wanyama
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
Kiswohil kidato cho kwanzo
+
Nomiono dhl
-Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika
kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika
wa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu
nyumba,vikombe vitabu na kadhalika Zile zisizohesabika
Vinavyohesabikavitanda,
hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maj
mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghalabu nomino hizo huwa sawa katika
uumoja na wingi
Nomino za kitenzi
-Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa,
iambishi {ku-) cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili
kukifanya kiwe nomino.
vi
umishi (V)
Vivimishi ni maneno yanayoclezea zaidi juu ya nomino, aghalabu vivumishi hutanguliwa na
‘nomino. Kuna aina kadhaa za vivumushi, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo.
Vivumis
vinaweza kyjitokeza katika aina tatu ndogondo;
Vivumishi vya if
hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza
kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile,
Vivumishi vy:
jvumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino. Kuna,
vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo
i ali.
kiujumla jumla bila kudhihirisha i
Vivumishi vya
bavyo huonyesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika
‘orodha,
Vivumishi vya kumiliki:-Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina mil
wana
stu au kitu kingine,
Vivumishi
yeshi:vivurnishi vya aina hii huonyesha mabali au upande kit
kilipo.
Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizifh}kwa vitu vilivyopo karibu na mziz
le}kwa
vitu vilivyo mbali
Vivumishi vya kuuliza:Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza
habari
ke. Hujibu sw
ni?ipi? ngapi?”
Vivumis
vya A- unge
:Vivumishi vy:
ina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a-
Kiusishi
hiki
hhuandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho
unganif.
huvumisha nomino iliyotajwa awali.Vivumishivya aina hii hutumika kuleta dhana z=—
Uni
iafasi katika orodha.
Vivumishi vya
kwa
ina:Hizi ni nomino zinazotumil
kama vivumishi ambazo
hhutumil
kufafannua nomino
Vivumi
‘vya pekee:Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo
huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi
ulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha
Mizizi vivumishi hivini:-ote, o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, ingineo.
-0-0t
juonyesha ujumla wa kitu au vitu
Kivumis
tha aina hii kina maana ya “ki
‘ila kubagua’
~enye:
ivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani,
senyew
ivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani
-Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha “tofauti na’ au “zaidi ya’ kitu Fulani
:Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi
or
Ttashele@ameil.com
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Vielezi(E)
Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo
kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi
Aina za vielezi
Vielezi vya Mahali
Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilifanyika. Aghalabu vielezi
hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza kiungo -NI mwishoni mwa neno
linaloashiria mahali.Kwa mfano:nyumbani, kazini, shuleni
mfano 1
‘+ Mtoto huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.
‘+ Msipitie sokoni mkienda kanisani.
Vielezi vya wakati
Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kinapofanyika; kwa mfano: jioni, jana, asubuhi, saa saba,
maka juz.
Mfano 2
+ Mzee Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao
+ Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku
+ Kisaka na Musa watakutana kesho
Vielezi vya Idadi
Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi.
Idadi Kamili:Viclezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika.
Kwa mfano:mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi
Mfano 3
‘+ Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia
‘+ Daktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini
siku mbili kwa mwezi
Idadi Isiyodhihirika:Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika
bila kutaja kiasi kamili kwa mfano:chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.
mfano4
+ Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.
+ Yeye hunipigia simu mara kwa mara,
Vielezi vya namna au jinsi
Vielezivya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo
vya aina kadhaa
Vielezi vya namna halisi
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja
katika uainishaji wa aina za maneno.
Vielezi vya namna mfanano
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
Kiswahili kidato cha kwanza
Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali.
Hujengwa kwa kuongeza kiambishi(ki-Jau kiambishi(vi-). Viambishi hivi hujulikana kwa jina la
viambishi vya mfanano. Mfano; Ulifanyavizurikumsaidia mwanangu.
Vielezi vya namna vikariri
Hivi nivielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili
Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleciambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika ali gani.
Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi nivieleci vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo
Vielezi vya namna viigizi
Hivi vinaelezea zaidi jinsitendo lilivyofanyika kwa)kuigiza au Kuftiatisha sauti inayojitokeza
wakati tendo linapofanyika au kutokea.
Vielezi vya wakati
Vielezivya namna hii huonyesha’ wakati wa kutendeka kwa\Kitendo.Huweza kutokea kama
maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi{p0.}
Vitenzi
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka, Kitenzi huarifu lililofanyika au
lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti
Aina za vitenzi
1. Vitenzi vikuu:Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha
sentensi.
2. Vitenzi visaidizi:Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile
uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo
vinavyobeba viambishi vya wakati
3. Vitenzi vishirikishi: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya
nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi
kishirikishi“ni” cha uyakinishina kitenzi shirikishi “si” si cha ukanushi
4. Vitenzi vishirikishi vikamilifu:Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na
hata hali. Kwa mfano:ndiye, ndio, ndipo.
Kazi za kitenzi kikuu
‘+ Kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa,
+ Kuonyesha wakati tendo linapotendeka
+ Kuonyesha hali ya tendo
+ Kuonyesha nafsi
+ Kuonyesha kauli mbali mbali za tendo
+ Kuonyesha urejeshi wa mtenda’mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za kitenzi kishirikishi
‘+ Kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
‘+ Kuonyesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani.
‘+ Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu
+ Kuonyesha sifa za mtu,
‘+ Kuonyesha umoja wa vitu au watu
‘+ Kuonyesha mahali
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
+ Kuonyesha msisitizo
+ Kuonyesha umilikishi wa kitu chochote,
‘Aina za wakati katika kitenzi
+ Wakati uliopita
‘+ Wakati uliopo
‘+ Wakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi
+ Hali ya masharti
‘+ Hali ya kuendelea kwa tendo
‘+ Hali ya kutarajia, kuamura na kuhimiza
Viwakilishi (W)
\Viwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina/nomino
Aina za viwakilishi
a. Viwakilishi vioneshi au viwakilishi vya kuonesha:Viwakilishi vionyeshi hutumika
badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja. Kwa
‘mfano; huyu, yule, hapo, kule, humo. Huyu si mwenzetu kabisa; kule hakufai kwenda
watoto.
b. Viwakilishi vya nafsi: Kwa mfano:mimi, wewe, yeve, sisi, nyinyi, wao
c. Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viuliziambavyo huashiriwa na mofu /kiambishi{-
pijambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Kwa mfano,
‘Wangapi wameondoka? Kipi kimekosewa?
4. Wiwakilishi vya urejeshiambavyo vinajengwa na shinaambapamoja na vipande vidogo
vidogo -ye-,-0- -cho-, vyo, 10, po, mo, kon.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli
‘ya majina yanayorejeshwa navyo. Mfano; aliyeondoko hatapewa chake.
e. Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza
kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
£ Viwakilishi_ vya pekee/vimilikishi:-Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha
rnomino, Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa. Mfano; ‘-angu, -ako,
-ake, -etu, -enu, -ao ‘, kwangu haingii megini, chako haikna thamani.
g. Viwakilishi vya A-unganifu:- Viwakilishi hivi huundwa kwa kihusishi chaA-
unganifukusimamia nomino iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au
znomino ya aina fulani. Kihusishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi
ambacho husimama mahali pa nomino. Mfano:ya _kwakeyamemshinda,vya
wazechaviguswi.
h. Viwakilishi vya sifa:Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika
setensi. Kwa mfano -cupe, -janja, tamu
i. Viwakilishi vya Idadi;[dadi Kamili- hutumia namba kuelezea idadi ya nomino. ‘saba,
‘mmoja, ishirini’ -Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake. Idadi
Isiyodhihirika- huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili: ‘chache,
nyingi, kadhaa, kidogo, wastani’
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Viunganishi
Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au
sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.
‘Aina za viunganishi
‘+ Viunganishi huru:hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya
vipashio vinavyoungwa. iunganishi huru hujumuisha:
+ Viunganishi nyongeza/vya kuongeza, kama vile, na, pia, pamoja. Baba na mwanae
wanacheza mpira, Alichukua chakula chote pamoja na akiba iliyokuwepo.
+ Viunganishi vya sababu/visababishi, mfano, kwa sababu, kwa kuwa, kwa vile,
madhali, ili. Alimsogelea karibu ila ambusu, Atatumikia kifungo madhali amebainika
‘kuwa na hatia.
+ Viunganishi vya uteuzi/ehaguo, Mfano; au, Naweza kwenda nyumani au shuleni.
+ Viunganishi vya kutofautisha/vya kinyumesila, lakini, kinyume na, japokuwa, ingawa,
ilihali. Mfano; Mkumbatie lakini usimbusu.
+ Viunganishi vya wakati.Wakati mfano; Mwalimu aliuliza swali wakati yeye amesinzia,
+ Viunganishi vya mashartisikiwa, iwapo, hadi, Mfano; utaruhusiwa kuingia hapa ikiwa
‘umevaa mavazi yanaostahili.
‘+ Viunganishi vihusishi; miongoni mwa, kati ya; mfano: Jane alikuwa miongoni mwa
washindi kumbi bora kitaifa,
+ Viunganishi tegemezizni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi
ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi hua ambavyo kwa pamoja huunda sentensi
changamano au shurtia. Mfano; -po-, -cho-, -o- Nili-po-amka…, Ali-cho-mwelez…,
alizo-o-neshwa….k
Vihusishi
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jingine. Vihusishi
aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi
‘+ Huonyesha uhusiano wa kiwakati; Mfano, ni vizuri kupiga mswakibaada yachakula
‘+ huonyesha uhusiano wa mahali: mfano, Ninaishikaribu nakwa Mtogole
‘+ huonyesha uhusiano wa kulinganisha: Amekulazaidi yauwezo wake.
‘+ -huonyesha uhusiano wa umilikaji: Usiguse hicho kitabu nicha kwangu
‘+ huonyesha uhusiano wa sababu kiini: nimerudi kwaajili yakuonana na mkuu wa shule.
Aina za vihusishi
a. vihusishi vya wakati
b. vihusishi vya mahali
cc. vihusishi vya vya kulinganisha
._vihusishi vya sababu
. vihusishi vya ala/kifaa mfano; -kwa
£vihusishi vimilikishi
g. vibusishi vya namna; Kichwacha mviringo
1h. vibusishi ‘na’ cha mtenda mfano, amepigwana Juma.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Matumizi ya kihusishi “kwa”
1. huonyesha mahali au upande: Mfano, amekwenda kwa mjomba wake.
2. huonyesha sababu au kisababishi cha jambo: mfano; ninaishi kwa ajili yako.
3. huonyesha wakati: mfano; sina nafasi kwa sasa.
4. huonyesha schemu fulani ya kitu kikubwa, mfano: Mpira umekwisha wakiwa
‘wamefungana nne kwa tatu.
5. huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka: Mfano; alimvuta kwa nguvu sana ndo maana
limevunjika.
Vihisishi/Viingizi
Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani.
Vihusishi vinaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:
Vihisishi vinavyoonyesha mhemko au hisi kali
a. vihisishi vya furaha
bb. vihisishi vya huzuni
cc. vihisishi vya mshituko
d._vihisishi vya mshangao
Vihisishi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio
a. vihisishi vya maadili
b. vihisishi vya mwiitiko
._vihisishi vya ombi
._vihisishi vya bezo
._vihisishi vya kutakia heri
£.vihisishi vya kukiri afya/jambo
. vihisishi vya kiapo
hh. vihisishi vya salamu
Matumizi ya aina za Maneno katika Tungo
Matumizi ya’Aina za Maneno katika Tungo
Elezea matumizi ya aina za maneno katika tungo
Aina za maneno hutumika katika tungo kwa kutegemeana na lengo la msemaji. Kwa mfano
kama lengo la msemaji ni kuonesha aina fulani ya hisia atatumia vihisishi katika tungo yake.
Vilevile kama msemaji anahitaji kucleza kubusu. namna nomino inayyotenda, ilivyotendewa au
inavyotendwa, atatumia kitenzi..
Matumizi ya Kamusi
Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa
jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo
‘wasomaji wanaweza kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika karatasi au nakala
tepe yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na maclezo mengine na kuhifadhiwa
katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wowote wa kielekroniki
Kamusi huweza kuwa ya lugha moja, yaani orodha ya maneno pamoja na maelezo yake yakiwa
katika lugha moja
Mfano 5
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Mfano:
chatuyni nyoka mkubwa na mnene
Kamusi nyingine huwa za lugha mbili yaani orodha ya maneno ipo katika lugha moja na
maelezo ya maana ya maneno hayo yapo katika lugha nyingine.
mfano 6
chatu,ipython
Kamusi ni hazina ya lugha inayohusika, kwani tofauti na vitabu vingine vya lugha, huwa na
orodha ya maneno mbali mbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha ile pamoja na maana
zake. Japokuwa wingi wa maneno hutegemea ukubwa wa kamusi, kitabu hiki kina manufaa
makubwa kwa mtumiaji/wake kwani humpatia msamiati asioufahamu pamoja na maana zake au
humpatia mana zaidi ya maneno anayoyafahamu.
Taarifa zinazopatikana katika kamusi
Awali_ kamusi zilipoanza kutungwa zilikuwa ni orodha ya manéno magumu pamoja na maana
zake, Kamusi za siku hizi huwa na taarifa zaidi ya maana. Miongoni mwa taarifa ambazo kamusi
huwa nazo ni:
‘+ tahajia za maneno mfano, Tasinifu Vs Tasnifit, Burangeti Vs Blanketi, Kula Vs Kura, –
ingine vs -engine
‘+ matamshi
‘+ sarufi ya lugha kama inavyojitokeza katika kila neno kama vile maumbo ya wingi wa
nomino, vinyambuo vya neno kama vile chezesha, chezeka, chezea, mchezo, mchezajin.k
ambavyo vinatokana na kitenzi cheza
‘+ etimolojia ya neno (asili ya neno husika)
‘+ matumizi ya neno
Jinsi ya Kutumia Kamusi
Maneno yanayoingizwa katika kamusi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno yanayoanza
na herufi a, yote huwekwa chini ya herufi A. Maneno yanayoanza na herufi fulani nayo
hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi ya pili, ya tatu, nne au tano ya neno
kama mfano hapa chini unavyoonyesha,
mfano 7
Mfano;ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi
Maneno yote yanaanza na herufi (j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya tatu ni [b]
na [d]. Kwa kuwa [b] hutangulia [4] katika mpangilio wa alfabeti maneno yenye [b] kabla ya
yale yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni mawili itabidi tutazame herufi ya nne ya
inya maneno ili tuchague litakaloorodheshwa mwanzo. Neno ‘jabali” litaorodhewshwa kabla ya
‘jabiri’ kwa kuwa [a] (herufi ya nne) ya ‘jabali? hutangulia (i) ya ‘jabiri” ambayo pia ni herufi ya
nne. Kisha tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya
nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya ‘jadhibika’ na ‘jadi’. Kwa kuwa [h]
hhutangulia (i] basi ‘jadhibika’ huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na ‘jadi’
Kwa hiyo hivi ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi ya
neno unalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya kwanza
kuorodheshwa.
Neno linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwakidahizo.Kidahizo huandikiwa
maelezo ya kukifafanua, Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana ya kidahizo, kategoria
ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo n.k. Kidahizo pamoja na maclezo yake
ridio huitwakitomeo cha kamusi.
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
Example 8
Kitomeo cha kamusi
Dhabihu (kidahizo)nm(kategoria ya neno) mahali pa kuchinjia wanyama (maana ya neno),
Taarifa Ziingizwazo katika Kamusi
Fafanua taarifa ziingizwazo katika kamusi
Maana za maneno
Kwa mfano:Dhabihunm mahali pa kuchinjia wanyama.
Kategoria za maneno
Kategoria za maneno kama vile kiclezi (cle), kitenzi (kt), kivumishi (kv), nomino (nm), kihisishi.
Mifano ya matumizi
Kwa mfano, Waiziraeli huwapeleka koondo wao kwenye dhabihu kwa ajili ya ondoleo la
dhambi. Lengo la kutoa mifano ni kumsaidia msomaji asiye fahamu vyema neno husika aclewe
jinsi neno hilo linavyotumika.
Uingizaji wa nomino
Nomino nyingi katika lugha ya kiswaili zina maumbo ya umoja na wingi.
Mfano:dumenmma-
mkoposnm mi-
Viambishi ambatishi huwekwa kando ya nomino kuashiria umbo la wingi la nomino,
Ngeli za nomino
Mfano:mkoponmmi- (u-/i=]
Kutafuta maana unayoitaka
Neno linaweza kuwa na maana moja au Zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji kamusi
hana tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno linapokuwa na maana Zaidi
ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi aichague. Ili kupata maana inayosadifi itafaa
‘mtumiaji kamusi kutafuta maana ambayo inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa.
Mfano:kifungonm vi-
1. kitu cha kufungia
2. kit kinachotumiwa kufungia vazi kama vile shati, gauni, survali n.k
3. adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa muda fulani
Iwapo mtumiaji aliona neno ‘kifungo” kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa kifungo cha
miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya kubaka….” Maana ya mukatadha hu itakuwa ni ile
maana ya 3 kwa sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo neno kifungo limetumika
nna wala sio maana ya | wala ya 2
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————