Kiswahili Form One Notes – Fasihi kwa Ujumla

Kiswahili Form One Notes – Fasihi kwa Ujumla

Full text version of Kiswahili Form One Notes on Fasihi kwa Ujumla, transcribed from the supplied source document. Source images are intentionally omitted; all recognized text from the topic pages is included below.

Full text: This page contains the complete recognized text for source pages 16-18. For the original PDF layout and illustrations, use the WhatsApp button below.
—————
‘Kiswahili kidato cho kwanza

MADA YA TATU: FASIHI KWA UJUMLA

Dhima ya Fasihi

Dhana ya Fasihi

Fasihi; ni sana ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake,
ndoto zake, matumaini yake, migogoro yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira yake.
(Wamitila, 2004).
Fasili hii imejaribu kufafanua vizuri kile ambacho fasihi inajihusisha nacho, kimsingi fasihi
inajihusisha na wanadamu. Vitu ya msingi tunavyoviona katika fasili hii ni kwamba fasibi ni
sanaa, na fasihi inatumia lugha lakini zaidi fasihi inajihusisha na wanadamu.

Dhima za Fasihi katika Jamii

Dhima za fasihi katika jamii ni pamoja na hizi zifuatazo:
+ Kuburudisha jamii:Pamoja na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii.
Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza
na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika,
+ Kuelimisha. Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii
wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa
kkuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi,
uubaya wa ufisadi na kadhalika.
+ Kuonya jamii, Fasihi ina jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa
‘maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya
kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii
+ Kuunganisha jamii Fasihi huleta watu katika jamii, Watu huunganishwa kupitia kazi
‘mbalimbali za kifasihi, kwa mfano, kupitia nyimbo, miviga, vichekesho na kadhalika.
+ Kukuza lugha.Fasihi hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi
huwa ni ya kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au
‘wasomaji. Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia
fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na
‘waandishi wa fasihi hubitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha.
+ Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii, Kupitia fasihi simulizi, tamaduni na
mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau na
vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika.
+ Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana
ili kupata suluhisho. Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika.

Aina za Fasihi

Kuna tanzu mbili za fasihi, ambazo ni fasihi andishi na fasihi simulizi

Dhana ya Fasihi Simulizi

Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sana ya lugha inayopitishwa kutoka
wa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.

Sifa na Dhima za Fasihi Simulizi

Sifa za Fasihi Simulizi

© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
—————
‘Kiswahili kidato cha kwanza
‘+ Hupitishwa kwa njia ya mdomo
‘+ Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika.
+ Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
+ Nimali ya jamii, Hakuna mtu falani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
+ Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu
hhutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
+ Aghalabu huwa na funzo fulan

Dhima za Fasihi Simulizi

+ Kuburudisha – Hufiyrahishia na kuchangamsha hhadhira
+ Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii
‘+ Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
+ Kutambulisha jamii – jamii mbalimbali husifika kutokana na’sanaa zao katika fasihi
simulizi kama vile nyimbo.
‘+ Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
+ Kuunganisha watu – huleta watu pamoja
+ Kukuza lugha – fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.
+ Kuliwaza – hutoa huzuni na kuleta matumaini
+ Kupitisha muda – wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda,
‘+ Fasihi simulizi ni chombo cha mawasiliano hususani kupitia ngomezi.

Dhana ya Fasihi Andishi

Fasihi Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno ya maandishi kupitisha ujumbe kwa
hadhira.
Kuna tanzu kuu nne za Fasihi Andishi:
1, Hadithi Fupi — Hii ni kazi ya fasihi andishi yenye kisa kimoja na mhusika mkuu mmoja
na maudhui yake sio changamani.
2. Riwaya -Ni kazi ya fasihi andishi yenye wahusika wengi na muundo changamani ni
ndefu na maudhui yake ni mapana
3. Tamthilia- ni kazi ya kisanaa yenye muundo wa kiugizikaji inayowasilishwa katika
‘maandishi
4. Mashairi – mashairi yakiwa yamechapishwa pia hutambulika kama fasihi andishi

Sifa na Dhima za Fasihi Andishi

Sifa za Fasihi Andishi

‘+ Hupitishwa kwa njia ya maandishi
+ Nimali ya mtu binafsi
‘+ Haiwezi kubadilishwa papo kwa papo
‘+ Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sana katika uwasilishaji wake.

Dhima za Fasihi Andishi

+ Kukuza lugha
+ Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
+ Kuburudisha
© twshole 2019 | twhvleegmeil.com
ji_——-—_—-——-——-—-—- —_—________————————
Ws 5
Kiswahil kidato cha kwanzo
+ Kuelimisha
+ Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
+ Kuonya, kuelekeza, kunasihi
‘Tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi
Zifvataz0 ni tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi kama zilivyobainishwa katika
jedwali hapa chins
| Ca ‘Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
‘mali va joni Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na
2. Ni mali ya jamii, Lehrer
3. Maimalizi anaweza Kubadilisha sehemt 14py klichoandikwa hakiwezi kubadilishwa
4, Huhifadhiwa akilini Huhifadhiwa vitabuni
5. Kazi simulizi hubadilika na wakati Kazi andishi haibadiliki na wakati
«6, Hluhitaji msimutizi na hadhira yake wawe Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi
‘mahali pamoja wakati wa masimulizi__peke yake, mahali popote, wakati wowote
7 pakusimutia Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na
– Miu yeyote anaweza kutunga na kusimulia, yey wa kusoma
3, Hutumia wahusika changamano (WwanyaMa,j5.ryiq wahusika wanadamu.
‘watu, mazimwi n.k)
© table 2019 | trhvle@amail.com
Ba es

GET ORIGINAL PDF NOTES THROUGH 255620339260

banner
Scroll to Top