Maelezo haya ya Kiswahili Form Two yanahusu Usimulizi wa Matukio. Yamepangwa katika sehemu zilizo wazi ili kurahisisha kusoma, kuelewa na kufanya marudio.
Usimuliaji wa Matukio
Njia za Usimulizi wa Matukio
Fafanua njia za usimulizi wa matukio
Usimulizi hufanyika kwa njia kuu mbili yaani kwa njia ya maandishi na kwa njia ya masimulizi ya mdomo. Kila njia hutegemea kwa namna msimuliaji anavyoweza kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa msimuliaji na msikilizaji hawakukaribiana, njia ambayo itatumika ni ile ya maandishi. Kwa mfano kama utahitaji kumweleza mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika kutumia maandishi, yaani utatumia njia ya kumwandikia barua.
Lakini kama unamsimulia mtu ambaye yupo karibu nawe, utatumia njia ya mazungumzo ya ana kwa ana.
Taratibu za usimulizi wa matukio
Usimulizi wa matukio dhamira yake ni kumweleza mtu au watu tukio ambalo wao hawakulishuhudia. Hivyo katika usimulizi msimuliaji hutakiwa kutoa maelezo muhimu ambayo yatawawezesha watu hao kulielewa tukio linalosimuliwa sawasawa na huyo anayeshuhudia. Mambo muhimu ya kutaja katika usimulizi wa matukio ni pamoja na haya yafuatayo:
1. Aina ya tukio — msimuliaji atatakiwa kubainisha katika maelezo yake aina ya tukio. Kwa mfano, kama ni harusi, ubatizo, ajali ya barabarani au mkutano.
2. Mahali pa tukio— ili msimuliaji aweze kuielewa habari inayosimuliwa, ni lazima kumwelewesha ni mahali gani tukio hilo limetokea. Kwa mfano, kama ni mjini inafaa kutaja hata jina la mtaa.
3. Wakati — katika usimulizi ni muhimu pia kutaja muda ambao tukio limetendeka kama ni asubuhi, mchana au jioni bila kusahau kutaja muda halisi yaani ilikuwa saa ngapi.
4. Wahusika wa tukio— ni muhimu kutaja tukio limehusisha watu gani, wingi wao, jinsia
yao, umri wao n.k.
Chanzo cha tukio— kila tukio lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa katika
usimulizi.
6. Athari za tukio— athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Kama ni ajali, je watu wangapi wameumia; wangapi wamepoteza maisha n.k.
7. Hatima ya tukio — msimuliaji katika usimulizi wake ni lazima abainishe baada ya tukio
kutokea na kushughulikiwa hatima yake ilikuwaje. Kwa mfano, kama tukio ni ajali ya
barabarani hatima yake inaweza kuwa majeruhi kupelekwa hospitalini na dereva
aliyehusika kukamatwa.
— eee
Kwa hiyo misingi hii ya usimulizi hufanya usimulizi wa tukio kuwa na schemu kuu tatu:
Utangulizi— schemu hii huwa na maelezo tu ya utangulizi ambayo hulenga kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji au wasikilizaji. Kwa kawaida utangulizi wa tukio huwa ni maneno machache kiasi yasiyozodi aya moja.
Kiini — kiini cha usimulizi huelezea tukio halisi kuanzia chanzo chake, wahusika, muda, mahali
na athari za tukio.
Mwisho— mwisho wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya mwisho ya tukio linalohusika, wakati mwingine matukio haya yanaweza kuambatana na maelezo ya msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio ambalo amesimulia.
Mbinu za usimulizi
Ili habari inayosimuliwa ipate kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za kusimulia katika hali inayovuta hisia za msikilizaji wake.
Baadhi ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi sahihi ya Kiswahili.
Kwa upande wa uigizi msimuliaji atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio ambalo anasimulia. Nayo ni kama vile milio, sauti na matendo.
Kwa upande wa usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti usimulizi huo uwe na kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa kwa maneno yasiyozidi matano, yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.
Kwa vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa katika
wakati uliopita.
Maelezo Ya Ziada
USIMULIZI WA MATUKIO
USIMULIZI
– Ni maelezo yanayotolewa kuhusu tukio au matukio yaliyotokea ambayo yanaweza kuwa mema au mabaya
AU
– Ni kitendo cha kutoa masimulizi juu ya mfululizo wa matukio yaliyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya msimuliaji. Mada hii lengo ni kumuwezesha mwanafunzi kutumia lugha ya Kiswahili fasaha kusimulia matukio mbalimbali.
– Katika usimulizi wa matukio ni lazima kuwe na msimuliaji na msikilizaji. Msimulizi lazima awe na sifa zifuatazo.
(a) Msimuliaji anatakiwa aweze kuwasilisha masimulizi yake kwa namna itakayochangamsha hadhira yake na ili aweze kufanikiwa juu ya hili, msimuliaji anatakiwa awe na kiwango cha hali ya juu cha ubunifu.
(b) Msimuliaji lazima awe na ufahamu mpana na lugha ya utamaduni unaohusika – hii husaidia katika kuwakilisha ujumbe vyema
(c) Pia inabidi msimuliaji awe mcheshi na awe anajua jinsi ya kuutumia ucheshi katika kunasa hadhira yake. Ucheshi huo lazima uhusiane na kile kinachowasilishwa na hadhira inayohusika.
(d) Msimuliaji anapaswa kuzifahamu tabia za binadamu pamoja na kuielewa mikondo mbalimbali ya jamii, pamoja na kufahamu mahitaji ya hadhira yake kwa sababu hadhira ya watoto huwa na vionjo, lugha yake na hata matarajio yake.
(e) Msimuliaji anapaswa kuwa na uwezo wa ufafanuzi na anayefahamu mbinu zifuatazo za sanaa na maonyesho.
• Ufafanuzi ni uwezo wa msimuliaji kuweza kuunda kugeuza na kuwasilisha kazi yake papo kwa papo bila ya kujiunga kwa muundo ni kama mabadiliko ya sauti, mikunjo ya uso n.k
• Kuna mbinu mbalimbali zinazotumika katika usimuliaji wa matukio. Utendaji ambao huwa na sifa kadhaa ambazo ndizo huitwa mbinu za usimuliaji wa masimulizi. Mfano wa sifa mojawapo ni uongozaji na umalizaji wa masimulizi, mara nyingi uongozaji huwa na mianzo maalumu, hisia za wasikilizaji pia huonyesha kuwa ni mwanzo wa masimulizi.
• Vilevile mwisho wake huweza kusaidia kupumzisha hadhira yake pia kama kuna mwasilishaji mwingine anayefuata huashiria kuwa anaweza akaanza kuhadithia.
Usimulizi wa matukio unasisitiza mtiririko mzuri wa visa pamoja na lafudhi sahihi ya Kiswahili.
Pia usimulizi wa matukio huzingatia;-
(ii)Matamshi – ili msikilizaji aweze kueleweka na kusikika vizuri mzungumzaji hana budi kusema kwa sauti, kuweka msisitizo panapostahili, kupambanua kauli yaani kama ni kauli ya kuuliza aulize na kama kauli ya taarifa aiseme kama kauli ya taarifa.
(iii) Utumizi wa lugha- msimulizi hana budi kujua anayezungumza naye kinachozungumzwa wakati na mahali anapozungumzia ili kuweza kutumia maneno kwa ufasaha na sio vizuri kuchanganya lugha.
(iv) Urefu wa habari – ni vizuri basi masimulizi yakawa mafupi ili yasimchoshe msikilizaji.
(v) Uhakika wa yale yanayosemwa- kwa kawaida masimulizi huwa na ushahidi wa yale yanayosemwa. Hivyo huusisha mifano dhahiri, hoja za msingi na mapendekezo ya kusaidia kama kuna tatizo.
Continue Studying Form Two
Get the Complete PDF Notes
Would you like these notes in a well-formatted PDF for easier reading and offline study? Click below to ask for the complete PDF notes.