Tenzi za Rohoni 103 – Kaa Nami

Tenzi za Rohoni 103 – Kaa Nami

Tenzi Na. 103

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 103, “Kaa Nami”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.
Siku zetu hazikawi kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho kaa nami.
Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa name.
Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.
Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote kaa nami.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top