Tenzi za Rohoni 102 – Kazi Yangu Ikiisha
Tenzi Na. 102
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 102, “Kazi Yangu Ikiisha”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.
Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.