Tenzi za Rohoni 101 – Twonane Milele

Tenzi za Rohoni 101 – Twonane Milele

Tenzi Na. 101

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 101, “Twonane Milele”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Nyimbo na tuziimbe tena
Za alivyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana!
Mbinguni twonane milele.
Twonane milele,
Twonane bandarini kule;
Twonane milele,
Twonane bandarini kule.
Hupozwa kila aoshwaye,
Kwa damu ya Kondoo yule;
Ataishi afurahiye
Vya Yesu mbinguni milele.
Hata sasa hufurahia
Tamu yake mapenzi yale,
Je, kwake tukifikilia,
Kutofarakana milele?
Twende mbele kwa jina lake,
Hata aje mwokozi yule,
Atatukaribisha kwake,
Tutawale naye milele.
Sauti zetu tuinue
Kumsifu Mwokozi yule,
Ili watu wote wajue
Wokovu u kwake milele.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top