Tenzi za Rohoni 104 – Twasoma Ni Njema Sana
Tenzi Na. 104
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 104, “Twasoma Ni Njema Sana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Twasoma, ni njema sana
Mbinguni, kwa Bwana;
Twasoma, dhambi hapana,
Mbinguni kwa Bwana;
Malaika wema wako,
Vinanda vizuri viko,
Na majumba tele yako,
Mbinguni kwa Bwana.
Siku zote ni mchana,
Ni nchi ya raha;
Wala machozi hapana,
Ni nchi ya raha;
Walioko wanuona
Uso wa Mwokozi, tena
Jua jingine hapana,
Ni nchi ya raha.
Nyama na vitu viovu
Havimo kabisa;
Kifo nacho, na ubovu,
Havimo kabisa.
Ni watakatifu wote,
Wameoshwa dhambi zote;
Wasiosafiwa wote
Hawamo kabisa.
Tuna dhambi, pia sote,
Mwokozi akafa;
Kwake tutaoshwa zote,
Mwokozi akafa;
Kwake twapata wokovu,
Tutawona utukufu;
Mbinguni tutamsifu;
Mwokozi akafa.
Baba, mama, ndugu zetu,
Twendeni kwa Bwana;
Huku chini sio kwetu,
Twendeni kwa Bwana;
Tusishikwe na dunia,
Na dhambi kutulemea;
Tutupe vya chini pia,
Twendeni kwa Bwana.