Tenzi za Rohoni 93 – Bwana Amefufuka

Tenzi za Rohoni 93 – Bwana Amefufuka

Tenzi Na. 93

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 93, “Bwana Amefufuka”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Bwana amefufuka, Aleluya.
Twimbe na malaika, Aleluya.
Sifa zetu na shangwe, Aleluya.
Na zao zisitengwe, Aleluya.
Ukombozi timamu, Aleluya.
Umetimu kwa damu, Aleluya.
Mshindi asifiwe, Aleluya.
Yu hai kwa milele. Aleluya.
Jiwe, lindo, muhuri, Aleluya.
Vi wapi? Na kaburi? Aleluya.
Kifo hakimuweki, Aleluya.
Ametoka peponi, Aleluya.
Yu hai mtukufu; Aleluya.
Cha kifo hatuhofu! Aleluya.
Alitufia sisi, Aleluya.
Tuwe mahuru nasi, Aleluya.
Kichwa chatangulia, Aleluya.
Tupae, nasi, pia!, Aleluya.
Kwa kuwa tuna fungu, Aleluya.
Mti, kaburi, mbinguni, Aleluya.
Ndiwe Mwokozi wetu, Aleluya.
Sifa ni yako Yesu, Aleluya.
Utukuzwe pekeo, Aleluya.
Ni wewe ufufuo, Aleluya.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top