Tenzi za Rohoni 94 – Siku Ya Mbingu Kujawa Na Nifa

Tenzi za Rohoni 94 – Siku Ya Mbingu Kujawa Na Nifa

Tenzi Na. 94

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 94, “Siku Ya Mbingu Kujawa Na Nifa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.
Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.
Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni mwokozi, kwake twaokoka.
Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele Mbinguni.
Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi: wangu, tutaonana.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top