Tenzi za Rohoni 92 – Nataka Nimjue Yesu
Tenzi Na. 92
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 92, “Nataka Nimjue Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake, na
Wokovu wake kamili.
Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake, na
wokovu wake kamili.
Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.
Nataka nifahamu, na
Nizidi kupambanua
Mapenzi yake, nifanye
Yale yanayompendeza.
Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake.