Tenzi za Rohoni 91 – Mapenzi Yako Yafanyike Bwana
Tenzi Na. 91
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 91, “Mapenzi Yako Yafanyike Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Mapenzi yako yafanyike,
Wewe mfinyanzi, nami towe,
Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.
Mapenzi yako yafanyike,
Unihoji dhambi zote,
Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo Msalabani.
Mapenzi yako yafanyike,
Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee, Mwokozi.
Mapenzi yako yafanyike,
Natoa kwako vitu vyote,
Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.
Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi yangu yavunjike,
Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.
Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale siku zote,
Sura ya Yesu umba kwangu,
Nijaze Roho nayo nguvu.