Tenzi za Rohoni 82 – Sioni haya kwa Bwana
Tenzi Na. 82
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 82, “Sioni haya kwa Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara!
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.
Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi,
Alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi.
Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.
Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.