Tenzi za Rohoni 83 – Kwa Wingi Wa Nyama

Tenzi za Rohoni 83 – Kwa Wingi Wa Nyama

Tenzi Na. 83

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 83, “Kwa Wingi Wa Nyama”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Kwa wingi wa nyama,
Na sadaka pia,
Hupata wapi salama,
Kwondoa hatia?
Sadaka ni Yesu,
Hwondoa makosa;
Dhabihu mwenye jina kuu,
Atanitakasa.
Kwa yangu imani,
Nikuweke sasa
Mkono mwako kichwani
Kukiri makosa.
Roho yakumbuka
Mambo ya mtini,
Mzigo ulijitweka,
Ndiyo yangu deni.
Deni hutanguka,
Tukimuamini;
Kwa damu tumeokoka,
Twimbe furahani.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top