Tenzi za Rohoni 31 – Msingi Imara
Tenzi Na. 31
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 31, “Msingi Imara”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Msingi imara, enyi wa kweli,
Umekwisha pigwa kwa neno hili;
Aongeze lipi? Mnayo pia
Kwa Yesu mliomkimbilia.
Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka taipunguza;
Takupa nawe, nikuwezeshe,
Ipata kufaa, isikutishe!
Utakapopishwa ndani ya moto
Nnguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.
Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni kwisha mapenzi yangu;
Nazo zitakapowenea, ndipo
Mabegani mwangu niwatwekapo.
Na mtu aliyenitegemea
Kamwe kwa adui sitamtia;
Nguvu za jehanam zijapotisha,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.