Tenzi za Rohoni 30 – Nilikuwa kondoo aliyepotea
Tenzi Na. 30
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 30, “Nilikuwa kondoo aliyepotea”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Nilikuwa kondoo aliyepotea,
Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
Nilikuwa mwana asiyesikia,
Sikupenda baba yangu wala kutulia.
Na mchunga mwema alinitafuta,
Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa,
Waliniona mnyonge, waliniokoa.
Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana,
Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana;
Kwa vidonda vyangu alitia dawa.
Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.
Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sasa nampenda Baba, na mchunga pia;
Kwanza nilitanga na kukosa sana,
Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.