Tenzi za Rohoni 32 – Yesu Awakubali

Tenzi za Rohoni 32 – Yesu Awakubali

Tenzi Na. 32

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 32, “Yesu Awakubali”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Wakosa
Yesu awakubali,
Wakosa, wahalifu,
Wambieni wa mbali
Habari ya wokovu.
Tangazeni kwa bidii,
“Akubali wakosa!”
Liwe neno dhahiri,
“Akubali wakosa!”
Awakubali Bwana
Neno lake amini
Watu kila aina
Waje kwake tengoni.
Mimi ni safi moyo
Na mbele ya sharia,
Aliye safi roho
Kwake ilitimia.
Akubali wakosa;
Nami anikubali;
Alivyonitakasa
Mbinguni niwasili.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top