Tenzi za Rohoni 26 – Yesu Unipendae
Tenzi Na. 26
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 26, “Yesu Unipendae”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Yesu unipendaye
Kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye,
Mwovu akinijia;
Yafiche ubavuni,
Mwako maisha yangu;
Nifiikishe mbinguni
Wokoe moyo wangu.
Ngome nyingine sina;
Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana ,
Nipe neema yako,
Ninakuamania
Mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia,
Vitani wanitosha.
Nakutaka Mpaji
Vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji,
Utanijazi vyako;
Nao waangukao
Wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao,
Uongoze vipofu.
Bwana umeniosha
Moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha
Yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona
Kisima cha uzima;
Mwangu moyoni Bwana,
Bubujika daima.