Tenzi za Rohoni 27 – Mungu Ni Pendo
Tenzi Na. 27
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 27, “Mungu Ni Pendo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Mungu ni pendo, apenda watu;
Mungu ni pendo, anipenda
Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda.
Nilipotea katika dhambi,
Nikawa mtumwa wa shetani.
Akaja Yesu kuniokoa,
Yeye kanipa kuwa huru
Sababu hii namtumikia,
Namsifu yeye siku zote.