Tenzi za Rohoni 24 – Mwokozi Moyoni Mwangu
Tenzi Na. 24
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 24, “Mwokozi Moyoni Mwangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu.
Amani moyoni mwangu,
kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu yeye,
Yu nami moyoni mwangu.
Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi wangu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu, Mwanawe Mungu.
Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
kwa kuwa ninaye Yesu.
Siogopi tena, nikiitwa kufa,
Yu nami daima, Yesu.
Mlango wa Mbinguni ni yeye pia,
“Tapita humo kwa damu.”
Nitaketi na yeye huko milele,
Nisifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.