Tenzi za Rohoni 23 – Ni Salama Rohoni Mwangu

Tenzi za Rohoni 23 – Ni Salama Rohoni Mwangu

Tenzi Na. 23

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 23, “Ni Salama Rohoni Mwangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

Ingawa shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top