Tenzi za Rohoni 16 – Kumtegemea Mwokozi
Tenzi Na. 16
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 16, “Kumtegemea Mwokozi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni.
Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kwake daima napata
Uzima na amani.
Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu,Mpendwa na Rafiki
Uwe nami dawamu.