Tenzi za Rohoni 17 – Namwadama Bwana

Tenzi za Rohoni 17 – Namwadama Bwana

Tenzi Na. 17

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 17, “Namwadama Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Namwadama Bwana kwa alilonena
Njia yangu huning’azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.

Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.

Giza sina kwangu wala hata wingu
Yeye mara huviondoa
Woga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki
Taamini nitii pia.

Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.

Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top