Kiswahili Form Two Notes – Uandishi

Maelezo haya ya Kiswahili Form Two yanahusu Uandishi. Yamepangwa katika sehemu zilizo wazi ili kurahisisha kusoma, kuelewa na kufanya marudio.

Insha za Hoja Insha za hoja ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia. Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake. Katika uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo. Ili hoja zote zipate kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana msimamo gani kuhusu mada hiyo. Muundo wa Insha za Hoja Elezea muundo wa insha za hoja Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:

1. Kichwa cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako.

Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya nk

2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.

3. Kiini cha insha;katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.

4. Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au

inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.

Barua Rasmi

Dhima ya Barua Rasmi

Elezea dhima ya barua rasmi

Barua rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni kutoa taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano kwa kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au marejeo.

Muundo wa Barua Rasmi

Elezea muundo wa barua rasmi

Barua rasmi au barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Kwa kawaida huwa na sehemu zifuatazo:

1. Anwani ya mwaandishi -huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa

karatasi. 2. Tarehe ya barua hiyo- tarche huandikwa chini ya anwani ya mwandishi

3. Anuwani ya mpokeaji- Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa

karatasi, na huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.

4. Salamu- Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => taja jina lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia. Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia bw/bi

5. Mada- Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe

mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.

6. Utangulizi- Hukaa chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maclezo mafupi yasiyozidi

aya moja ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo. 7. Ujumbe- Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.

8. Tamati- mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako mwaminifu, [jina], Sahihi

Simu

Dhima ya Simu ya Maandishi

Elezea dhima ya simu ya maandishi

Simu za maandishi ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana kuliko barua za kawaida.

Simu hizo huandikwa kwenye fomu maalumu ambazo hutolewa na shirika la posta. Simu za maandishi hujulikana kama telegram.

Kwa kawaida simu za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika simu za maandishi ni njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya kuandika simu yako ujumbe humfikia huyo unayemtumia katika muda usiozidi siku tatu.

Gharama za simu za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika. Kwa hiyo ujumbe unaotumwa huandikwa kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama kubwa. Example 1

Mfano wa simu ya maandishi:

| Musa Kingambe Slp 5299 Dsm

NJOO HARAKA

DADA MGONJWA LINGIDO

Kuandika Simu za Maandishi kwa Kuzingatia Muundo na Taratibu za Uandishi

| Andika simu za maandishi kwa kuzingatia muundo na taratibu za uandishi Muundo wa kuandika simu za maandishi una mambo yafuatayo ya kuzingatia ambayo ni anwani | ya mpelekewa taarifa, ujumbe na jina la mwandishi au mtuma simu. Mambo mengine ya kuzingatia ni kuandika maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha usomaji na kuandika simu ya maandishi katika karatasi maalumu ambayo hutolewa na posta. Activity 1

Andika simu za maandishi kwa kuzingatia muundo na taratibu za uandishi Kadi za Mialiko

| Kadi za mialiko ni aina ya karatasi ngumu zinazopeleka taarifa fupi za kumwomba mtu ahudhurie katika sherehe fulani kama vile harusi, ubatizo mahafali n.k Muundo wa Kadi ya Mialiko

Fafanua muundo wa kadi ya mialiko

| Mambo muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa katika kadi ya mwaliko:

1. Jina la mwandishi au mwalikaji

2. Jina la mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama vile: Profesa, Bi., Bw. Bw&Bi nk

  1. Lengo la mwaliko
  2. Mahali pa kufanyika shughuli

5. Tarehe ya mwaliko

6. Wakati wa shughuli

7. Jina na anwani ya mtu atakayepelekewa majibu.

Mialiko huweza kuandikwa kwa namna mbili yaani kama barua au kadi. Jina la mwalikwa katika

| kadi ya mwaliko hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama vile Bwana….Bi….. Ndugu…ikiwa waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na Bwana na Bibi. Example 2

Mfano wa Kadi ya Mwaliko

Familia ya Manyama na Joseph

| Wanapenda —kukualika/kuwaalika _Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi……… kwenye

harusi ya kijana wao mpendwa Benny Joseph itakayofanyika huko Kiabakari katika ukumbi wa simba siku ya Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana hadi saa 3.00 usiku

Kufika kwako ndio mafanikio ya sherehe hii.

Majibu kwa (wasiofika tu)

Emmanuel Joseph

  • Simu: 0786 67 54 62 Uandishi wa Dayalojia Dhana ya Dayolojia Elezea dhana ya dayolojia Dayalojia ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanaozungumza kwa kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utunagaji, dayalojia inaweza kuwasilishwa kwa nijia ya mazungumzo au maandishi. Katika kutunga dayalojia mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa mfano kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi. Mambo ya kuzingatia katika dayalojia ni pamoja na haya yafuatayo:
  • Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha
  • Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
  • Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimua
  • Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia iwe na uhalisia. Example 3 Mfano wa dayalojia (Anaonekana mwenye furaha,anamwita rafiki yake, Anna)Wow, Anna! Tumekutana Wambura: tena, siamini macho yangu! (wanakumbatiana wote wakiwa na nyuso za furaha). (Anatabasamu huku ameshikilia mkono wa kulia wa Wambura, anaonesha shauku kuu)Wambura! Bado unanikumbuka? Nina furaha sana kwa kweli, ni muda mrefu Anna: sana. (Anachekelea) Aaaah, nahisi kama naota Neema, siamini kama nimekutana na wee leo

Wambura: hii ni muda mrefu sana, nimefurahi kwa kweli. Anna: (Anachekelea)

Wambura: Mbona wachekelea tu….

Maelezo Ya Ziada

Shairi huimbwa au kusomwa na mtu Ngonjera husemwa na watu wawili au mmoja zaidi wanaojadili matatizo mbalimbali.

  • Maneno yake hulenga kujibu swali
  • Maneno ya mashairi hutofautiana
  • moja
  • kutoka shairi hadi shairi, dini, majonzi,
  • matatizo ya siku kwa siku

– Mara nyingi mwisho wanangonjera huishia na mshindi na dhamira itakiwayo.

– Ni pia wakati mwingine watu huona kama udhaifu kwani inapasua pande zote mbili zijadiliwe kwa kina na kwa usawa. Upande wa kufaulu na kutokufaulu.

UANDISHI

Insha

– Ni mfululizo wa sentensi zinazohusiana na mada inayozungumziwa au kuandikwa. Uandishi wa insha huwa katika haya.

Kuna aina kuu mbili za insha

(a) Insha za wasifu

(b) Inshaza hoja

– Lakini pia insha hizi zinagawanyika tena mara mbili. Insha za wasifu za kisanaa na zisizo za kisanaa

– Insha za wasifu za kisanaa huwa na lugha ya mvuto na misemo kama nahau methali na tamathali za semi mbalimbali.

– Insha za wasifu zisizo za kisanaa. Ni insha ambazo huwa na lugha ya kawaida.

Insha za hoja

– Ni insha ambazo hutetea mawazo ya aina fulani na kupinga mengine kwa uthibitisho uliodhahiri. Insha hizi huonesha ubora na udhaifu wa mawazo yanayojadiliwa.

– Unapoandika insha za hoja hakikisha unapanga mawazo katika mtiririko unaofaa ili hoja zake zipate nguvu na kukubaliwa.

– Kunakuwa na pande mbili zinazopingana. Moja ikiunga mkono na moja ikikataa.

– Uelewa wa mada inayojadiliwa ni muhimu. Mwandishi awe na msamiati wa kutosheleza lugha sanifu na fasaha huku ukizingatia na sarufi ya lugha husika.

Hatua za uandishi wa insha

(a) Kichwa cha insha

– Hiki huandikwa kwa herufi kubwa katika juu na mara nyingi huwa hakizidi maneno matano (5). Kichwa cha insha huandikwa muhtasari kwa kuzingatia wazo kuu la insha na mara nyingi hupigiwa mstari.

(b) Utangulizi wa insha

– Huu huzingatia fasihi ya jambo linalozungumziwa, uhusiano wake na vitu vingine na muhtasari wa insha inayotungwa.

(c) Kiini cha insha

– Hii ndio sehemu kuu ya insha ambapo mwandishi anapaswa afafanue kwa mapana mada inayoelezwa huku akitoa mifano hai inayoendana na hali halisi. Kila haya huwa na wazo kuu moja.

(d) Hitimisho la insha

– Katika sehemu hii mwandishi anapaswa kutoa mapendekezo (maoni) ya msingi au kusisitiza. Kwa ufupi yale aliyoyaeleza katika habari yenyewe.

UANDISHI WA BARUA

Barua rasmi – Hii ni aina ya barua ambayo huandikwa kwa makusudi maalum.

Dhima za barua rasmi

– Kuomba kazi au huduma

– Kuagiza na kupokea vifaa

– Kutoa taarifa mbalimbali kama vile kushindwa kufika mkutanoni kuomba kiwanja, mkopo

– Kutuma pongezi kwa aliyefanya vizuri kazini

Barua za kikazi zipo za aina nyingi lakini zinaweza kugawanywa katika mafungu matatu nayo ni: –

(a) Barua za taarifa

(b) Barua za maombi ya kazi/ huduma

(c) Barua za uagizaji na upokeaji wa vifaa.

– Barua za kikazi huandikwa kuelezea ujumbe maalum kwa hiyo huhitaji kuandikwa kwa makini na uangalifu wa kutosha. Ni muhimu kuandika waziwazi jambo lililokusudiwa.

– Mwandishi analazimika kuandika kwa ufupi na kwa lugha nyepesi, ni muhimu kuepuka maelezo yasiyo muhimu. Mara zote barua za kazi huwa na sentensi fupi, sentensi chache na zenye maana

Muundo Wa Barua Ya Kikazi

1. Anuani ya mwandishi

– Lazima mwandishi aandike anuani yake , iwe juu kwenye pembe ya mkono wa kulia wa karatasi. Hii inatakiwa iandikwe kikamilifu na kwa usahihi.

2. Tarehe

– Pia huandikwa mkono wa kulia wa karatasi barua, chini ya anuani ya mwandishi

3. Kumbukumbu namba

– Barua za kikazi ni lazima ziwe na kumbukumbu namba ya kuitambulisha. Mara nyingi kumbukumbu namba huwa na tarakimu au herufi au vyote kwa pamoja.

– Kumbukumbu namba hii ni kama jina la kutambulisha barua hiyo katika majibu au mfululizo wa majibizano

4. Anuani ya mwandikiwa

– Mara zote hutangulia na cheo cha mwandikiwa upande wa kushoto chini ya kumbukumbu namba. Nafasi kidogo huachwa baina ya kumbukumbu namba na anuani hii.

5. Mwanzo wa barua

– Katika sehemu hii ni heshima kutaja cheo cha mwandikiwa mfano; Ndugu katibu, Ndugu afisa mifugo, Ndugu mkuu wa shule, na huandikwa chini ya anuani ya mwandikiwa.

6. Kichwa cha habari

– Lazima barua ya kikazi iwe na kichwa cha habari kinachotaja kwa ufupi jambo linalohusu barua, kichwa cha barua huandikwa katikati ya barua mara baada ya mwanzo wa barua. Ni muhimu kiwe kifupi na chenye kueleweka waziwazi. Ni lazima kipigiwe mstari na kuandikwa kwa herufi kubwa.

7. Barua yenyewe

– Katika sehemu hii huandikwa mambo yote muhimu yanayohusu barua hiyo na taarifa zilizo dhamiriwa tu. Kwa sababu uanzaji wa barua yenyewe humrejesha msomaji kwenye maadili kufupisha maelezo kama vile: –

– Rejesha maongezi yetu ya juzi, mada hii inahusika, rejea mada hapo juu, barua yako ya tarehe.

8. Mwisho wa barua

– Sehemu hii ni tamko la heshima la kumalizia barua, mara nyingi mwisho unaotumika katika barua ya kikazi ni kama vile wako mtiifu, wako mwanachama/ mwanakijiji, wako katika ujenzi wa taifa, wako katika kazi n.k.

9. Saini na jina la mwandishi

– Mwisho wa barua mwandishi aweke saini na jina lake. Kama barua imechapwa basi itambidi aweke sahihi kwa mkono.

1. Cheo cha mwandishi wa barua

– Mwisho wa barua mwandishi aweke saini na jina lake kama vile katibu kata, waziri wa elimu, mjumbe wa shina.

Barua Za Kikazi Za Taarifa

– Barua za kikazi za taarifa zinaweza kutoa taarifa fulani kama vile msiba, onyo, kushindwa kufika shuleni, mkutanoni, wizi uliotokea kijijini. Mara nyingi barua ya taarifa huweza kuwa na ombi.

– Ni muhimu kukusanya barua zote zinazohusu jambo hilo litamwelewesha kikamilifu anayeandika.

Mfano wa barua ya taarifa kuhusu “tatizo la simba

kijijini''

Kijiji cha kafule

S. L. P 9

Itumba

20/08/1999

Bwana nyama ya Wilaya

S. L. P 10

Itumba

Ndugu;

Yah: Tatizo La Simba Kijijini

Husika na kichwa cha barua hapo juu. Ninasikitika kukutaarifu kuwa hapa kijijini kwetu amezuka simba anayewinda watu. Ni simba jike na ana watoto watatu na ameonekana mara tatu hapa kijijini.

Simba huyo huingia hapa kijijini kutoka katika msitu wa hifadhi ya Taifa Ambasi. Tunaomba ruhusa yako tuweze kuweka mtego. Nitashukuru kama mtashauri jambo la kufanya mara utakapopata barua hii.

Wako katika kazi,

K.Makosi

Kamwene makosi

Mtendaji wa kijiji.

– Vile barua hii ya kikazi za taarifa wakati mwingine inaweza ikawa inatoa taarifa za mwaliko wa masuala mbalimbali kama sherehe, mkutano kuanzisha mradi fulani, kufungua jingo.

– Barua hii hueleza waziwazi kusudi la kuandikwa, tarehe, wakati mahali itakapofanyika. Mfano wa barua.

Shule ya Sekondari Buza

S.L.P 30 Tanga

10/09/2000

Mkuu wa shule

Wilaya ya Tanga mjini

S. L. P 300

Tanga

Ndugu,

YAH: OMBI LA MWALIKO WA KUKABITHI VYETI VYA KUMALIZA KIDATO

CHA SITA (6)

Husika na kichwa cha habari hapo juu. Ninakualika uwe mgeni rasmi ili kukabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya kidato cha sita kwa wahitimu 600 katika shule ya Buza tarehe 20/09/2000. Kufika kwako ndiyo kufanikisha shughuli hiyo . sherehe hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni

Nitashukuru sana iwapo ombi letu litakubaliwa

Neeba Nsi Yomo

Barua Ya Maombi Ya Kazi

– Barua hii inahitaji iandikwe kwa uangalifu zaidi. Huandikwa kwa ufupi na huandikwa mambo yaliyo muhimu tu mfano kiwango chako cha elimu.

– Kuna mambo mnne yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuandika barua ya kuomba kazi nayo ni: –

(a) Kutaja kazi unayoomba

– Sehemu hii ni lazima mwandishi ataje bayana kazi anayoomba ili msomaji asipate shida kutambua aina ya kazi anayohitaji.

(b) Elimu na ujuzi

– Ni muhimu mwandishi kueleza sehemu na viwango mbalimbali vya elimu alivyonavyo na pia kutaja kwa majina ya shule pamoja vyuo alivyosoma.

– Vilevile ni vizuri kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi pamoja na nakala za vyeti vyako na hata kama cheti kinachothibitisha ujuzi wako.

(c) Maelezo binafsi kwa ufupi

– Ni muhimu pia kueleza mambo binafsi kama vile kuelewa umri kama muombaji ameoa au hajaolewa, vipaji alivyonavyo mwombaji au kama ana mambo mengine anayopendelea kama vile sanaa, uandishi, michezo, muziki.

(d) Wadhamini

– Pia mwombaji anapaswa kutaja majina ya watu ambao wanaweza kutoa taarifa zaidi kuhusu elimu tabia na hata ujuzi wake.

– Na watu hawa wanaweza kuwa waalimu wake wa shule au vyuo, mwajiri wake wa zamani,au kiongozi yoyote lakini ndugu au rafiki hairuhusiwi kuwa wadhamini.

BARUA YA UAGIZAJI NA UPOKEAJI VIFAA

Mfano wa barua ya kupokea vifaa

Kijiji cha Mkwawa

S. L. P 180

Iringa

28/12/2000

Meneja wa kiwanda

Kiwanda cha zana za kilimo Mbeya

S. L. P 4000

Mbeya

Ndugu,

Yah: Kupokea Vifaa Vya Kilimo

Rejea barua yetu ya tarehe 15/12/2000. Ninayo furaha kukufahamisha kuwa vifaa ulivyotuma vimetufikia. Tumepokea vifaa vifuatavyo:

  1. Majembe – 6
  2. Toroli – 1
  3. Slasha – 20
  4. Mapanga – 10
  5. Mashoka – 6

Vifaa hivi vikefika salama na viko katika hali nzuri na mradi umekwisha anza na tunakukaribisha kututembelea upatapo nafasi ili uone tunavyoendesha mradi huu

Wako katika kazi

P.Kaboka

Pambula Kaboka

Mratibu wa mradi

Kadi Za Mialiko

– Hizi ni barua au kadi ziandikwazo kwa ajili ya kumualika mtu ahudhurie sherehe au kikao fulani.

– Jina la mwandishi na anuani yake

– Jina la mwandikiwa au mwalikwa

– Lengo la mwalikaji kwa ufupi

– Tarehe ya mwaliko

– Mahali pa kukutania

– Wakati wa kukutania

– Jibu lipelekwe kwa nani

Uandishi Wa Barua Za Simu

– Simu za maandishi ni njia mojawapo ya mawasiliano ya haraka baina ya mtu na mtu. Mwandikiwa hupata taarifa haraka iwezekanavyo ukilinganisha na barua za kawaida.

– Taarifa ya simu ni fupi lakini ina ujumbe ulio wazi na unaoeleweka. Ufupi wa simu za maandishi unatokana na gharama kubwa za malipo kwa sababu gharama za simu hulipwa kulingana na idadi ya maneno yaliyoandikwa.

Barua za simu zipo za aina mbalimbali kama vile

(a) Barua za simu ya kawaida

(b) Barua ya simu ya kupeleka fedha

(c) Barua ya simu ya haraka

Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa barua za simu

• Anuani ya mpelekewa habari o Anuani ya barua ya simu lazima iwe kamili na ya wazi kuwezesha barua hiyo kupelekwa kwa haraka iwezekanavyo bila matatizo. Pia anuani ya mji unapokwenda ni muhimu ikiwezekana na mtaa na namba ya nyumba

• Taarifa au ujumbe o Mara nyingi ujumbe huwa na maneno machache pia habari ielezwe kwa ufupi mno na iwe inaeleweka lakini epuka maelezo yasiyo ya lazima.

  • Jina la mwandishi
  • Hakikisha unaandika kwa herufi kubwa barua yako ya simu
  • Kutoweka alama yoyote kama vile mkato, nukta n.k
  • Simu zenye taarifa zaidi ya moja zitengwe kwa kutumia nukta
  • Maandishi yote yanatakiwa yawe kwenye fremu.

Matumizi ya simu za maandishi ni kutoa taarifa mbalimbali kama:

Taarifa juu ya kifo, juu ya ugonjwa, taarifa juu ya kufaulu mitihani, kutoa taarifa juu ya kupata kazi, kutoa taarifa juu ya kujiunga na shule, taarifa juu ya safari n.k

Dhima za simu za maandishi

  • Kutoa taarifa za kilio, ajali au tukio lolote la ghafla kwa haraka, wazi, ufupi na huku zikieleweka.
  • Kupata majibu ya haraka
  • Hii ni pale kwa mtumiaji anapolipia majibu na kuandika maneno R.P (Reply paid) kabla ya jina la mpelekewa simu

Mfano wa barua ya simu

SHABANI MUSA SLP 54 KILIMANJARO NITUMIE 20000 YA MTIHANI PAMELA

MISOSI

Uandishi Wa Dayolojia

Dayolojia

– Ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi.

– Dayolojia yaweza kuwasilishwa kwa njia ya mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi.

– Katika utungaji wa dayolojia mtunzi hana budi kujifanya kama muhusika mwenyewe. Vilevile mtunzi anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudiwa kuandika

– Pia anapaswa kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko wa kufurahisha wahusika. Hali kadhalika awapangie wahusika majukumu kulingana na matendo yao.

– Mfano kama mhusika ni mkulima basi lugha atakayopewa, vifaa hata mandhari iliyomo vifanane au viwe kama mkulima halisi.

Mambo ya msingi katika utunzi wa dayolojia

(i) Mazungumzo ya mhusika lazima yawe mafupi ili yakumbukwe na yasimchoshe msomaji au msikilizaji.

(ii) kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha msomaji na msikilizaji mambo yanayotendeka mfano (anasimama ghafla kwa hasira).

(iii) kutumia vihisishi mfano Lo! Ati!, kweli!, n.k ili kuifanya dayolojia iwe ya kusisimua.

(iv) Pawepo na mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayolojia iwe na uhalisia mfano anaweza kutumia (………)

(v) Lazima lugha inayotumika na mtunzi izingatie sarufi lakini lugha au maneno ya wahusika yatategemea shughuli walizopewa.

Mfano wa dayolojia

(Akiwa na uso wa hasira, mama anamwita binti yake)

Mama : (akiita) Rose, Rose!

Rose : Nini tena?

Mama : Njoo hapa haraka

Rose : (anakuja polepole) nimekuja haya sema

Mama : Nieleze ulilala wapi?

Rose : Mbona wewe sijakuuliza ulilala wapi?

Mama : Unasemaje?

Rose : kwani hukusikia, unataka faida

Mama : (anahamaki) kweli mtoto wewe ni ibilisi, shetani

Mkubwa…………….

Rose : Umemaliza matusi yako? Nitahama humu ndani

Mama : (amepiga mayowe ya hasira huku anamfukuza Rose)

Haya toka ndani na usirudi tena hata siku ya

mazishi yangu…………..

Rose : (anamtazama mama yake kwa dharau) acha presha.

Continue Studying Form Two

Get the Complete PDF Notes

Would you like these notes in a well-formatted PDF for easier reading and offline study? Click below to ask for the complete PDF notes.

GET WELL-FORMATTED PDF NOTES

View More Secondary School Notes

banner
Scroll to Top