Tenzi za Rohoni 65 – Safari
Tenzi Na. 65
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 65, “Safari”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Katika safari yetu
Kwenda Mbinguni
Tusiishe siku zetu
Usingizini.
Ng’oani! Tujifungeni,
Twende zetu juu!
Kristo ndiye kiongozi;
Tusihofu tu.
Atwekwe badala yetu,
Mwenyewe Bwana;
Yesu kiongozi wetu
Atapokea.
Kisimani, maji tele,
Maji mazima!
Maji hayo,
Ya milele
Yana neema.
Njiani miiba mingi,
Yatuumiza;
Hofu na hatari nyingi,
Sana zakaza.
Kweli, njia ya Mbinguni
Ni ya mashaka;
Tuwe na Yesu njiani,
Mara hufika.