Tenzi za Rohoni 64 – Ujaribiwapo, Sifanye Dhambi
Tenzi Na. 64
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 64, “Ujaribiwapo, Sifanye Dhambi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Ujaribiwapo, sifanye dhambi,
Bali uzishinde, kwa Yesu kutii.
Fuliza kiume ushinde tamaa;
Yesu ni Mwokozi, hukuokoa.
Umwombapo yu papo
Akuongeze nguvu,
Atakusaidia;
Yesu atakufaa.
Wepushe waovu, matusi dharau;
Heshima la Mungu, kamwe sisahau;
Fanya uhodari, uwe mpole,
Atakuokoa hata milele.
Avumiliaye hupewa taji;
Tujaposumbuka tu washindaji,
Na mwokozi wetu hutuwezesha
Tusiwe kushindwa kama twakesha.