Tenzi za Rohoni 46 – Twae Wangu Uzima

Tenzi za Rohoni 46 – Twae Wangu Uzima

Tenzi Na. 46

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 46, “Twae Wangu Uzima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na siku,
Zikutukuze huku.
Twae mikono nayo
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu
Kwa wongozi wako tu.
Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.
Twae dhanabu pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.
Nia itwae, Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako.
Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Nniwe wako halisi.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top