Tenzi za Rohoni 45 – Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu

Tenzi za Rohoni 45 – Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu

Tenzi Na. 45

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 45, “Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu
Wala usifanye tashwishi.
Tazama! Tazama! Tazama uishi!
Mtazame huyo aliyeangikwa juu
Hivi sasa upate ishi.
Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi,
Na makosa yako maovu!
Kama deni zetu zote hakulipa
Mbona imemwagika damu?
Si kutubu na sala ikomboayo,
Ila damu ndiyo salama;
Na aliyeimwaga aweza, sasa,
Dhambi zako kukufutia.
Usiwe na shaka, Mungu amesema,
Hakuna alilolisaza;
Hapo alipokuja alitimiza
Kazi zote alizoanza.
Basi twae uzima, kwa kufurahi
Upokee kwa Bwana, sasa;
Ujijue hakika kwake kuishi
Yesu aishiye kabisa.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top