Tenzi za Rohoni 12 – Ewe Roho wa Mbinguni

Tenzi za Rohoni 12 – Ewe Roho wa Mbinguni

Tenzi Na. 12

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 12, “Ewe Roho wa Mbinguni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ewe Roho wa Mbinguni
Uje kwetu sasa.
Ufanye makazi yako
Ndani ya Kanisa.

Ndiwe mwanga, umulike
Tupate jikana;
Mengi kwetu yapunguka,
Tujalize, Bwana.

Ndiwe Moto, teketeza
Taka zetu zote:
Moyo na iwe sadaka
Ya Mwokozi, yote.

Ndiwe Umande, na kwako
Tutaburudika,
Nchi kavu itakuwa
Ni yenye Baraka.

Roho wa Mbinguni uwe
Nasi hapa chini,
Mwili uufananishe
Na kichwa Mbinguni.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top