Tenzi za Rohoni 13 – Tafuta daima utakatifu

Tenzi za Rohoni 13 – Tafuta daima utakatifu

Tenzi Na. 13

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 13, “Tafuta daima utakatifu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na Wakristo tu;
Nena siku zotena Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.

Tafuta daima utakatifu;
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.

Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako aew Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako;
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top