Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 85 – Ni “Mtu Wa Simanzi”

Tenzi za Rohoni 85 – Ni “Mtu Wa Simanzi” Tenzi Na. 85 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 85, “Ni “Mtu Wa Simanzi””, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Ni “Mtu wa Simanzi”, Mwana wa mwenye enzi Mwenye mengi mapenzi! Asifiwe Bwana Yesu! Akawa matesoni, “Mungu mwana yakini Akatoka Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu! Akapata dhihaka, Mzoea – mashaka Ndiye yetu sadaka: Asifiwe Bwana Yesu! Tu wenye dhambi sana; Kwake dhambi hamna, Na Mungu twapatana: Asifiwe Bwana Yesu! Alikufa mtini, Akalia dhikini, Sasa yuko Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu! Punde atarejea, Yesu kutunyakua, Ndipo tutamwimbia: Asifiwe Bwana Yesu! ← Tenzi 84 | Tenzi Zote | Tenzi 86 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 84 – Niwonapo Mti Bora

Tenzi za Rohoni 84 – Niwonapo Mti Bora Tenzi Na. 84 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 84, “Niwonapo Mti Bora”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Niwonapo mti bora Kristo aliponifia Kwangu pato ni hasara Kiburi nakichukia. Na nisijivune, Bwana Ila kwa mauti yako; Upuzi sitaki tena, Ni chini ya damu yako. Tangu kichwa hata nyayo, Zamwagwa pendo na hamu, Ndako pweke hamu hiyo, Pendo zako zimetimia. Vitu vyote vya dunia, Si sadaka ya kutosha; Pendo zako zinawia Nafsi, mali, na maisha. ← Tenzi 83 | Tenzi Zote | Tenzi 85 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 83 – Kwa Wingi Wa Nyama

Tenzi za Rohoni 83 – Kwa Wingi Wa Nyama Tenzi Na. 83 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 83, “Kwa Wingi Wa Nyama”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Kwa wingi wa nyama, Na sadaka pia, Hupata wapi salama, Kwondoa hatia? Sadaka ni Yesu, Hwondoa makosa; Dhabihu mwenye jina kuu, Atanitakasa. Kwa yangu imani, Nikuweke sasa Mkono mwako kichwani Kukiri makosa. Roho yakumbuka Mambo ya mtini, Mzigo ulijitweka, Ndiyo yangu deni. Deni hutanguka, Tukimuamini; Kwa damu tumeokoka, Twimbe furahani. ← Tenzi 82 | Tenzi Zote | Tenzi 84 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 82 – Sioni haya kwa Bwana

Tenzi za Rohoni 82 – Sioni haya kwa Bwana Tenzi Na. 82 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 82, “Sioni haya kwa Bwana”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Sioni haya kwa Bwana Kwake nitang’ara! Mti wake sitakana, Ni neno imara! Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo; Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo. Kama kiti chake vivyo Ni yake ahadi, Alivyowekewa navyo Kamwe havirudi. Bwana wangu, tena Mungu Ndilo lake jina! Hataacha roho yangu Wala kunikana. Atakiri langu jina, Mbele za Babaye, Anipe pahali tena Mbinguni nikae. ← Tenzi 81 | Tenzi Zote | Tenzi 83 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 81 – Chini Ya Msalaba

Tenzi za Rohoni 81 – Chini Ya Msalaba Tenzi Na. 81 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 81, “Chini Ya Msalaba”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Chini ya msalaba Nataka simama; Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema; Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu Wakati wa hari. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili; Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli; Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani, Msalaba umekuwa Ngazi ya Mbinguni. Na Yesu msalabani Walimkemea, Alikufa niokoke Niliyepotea; Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda, Nisiyestahili. Atakayeonana, Na Yesu Mbinguni, Njia yake aanzapo Ni msalabani; Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana, Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana. ← Tenzi 80 | Tenzi Zote | Tenzi 82 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 80 – Wamwendea Yesu kwa kusafiwa

Tenzi za Rohoni 80 – Wamwendea Yesu kwa kusafiwa Tenzi Na. 80 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 80, “Wamwendea Yesu kwa kusafiwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Wamwendea Yesu kwa kusafiwa, Na kuoshwa kwa damu ya kondoo? Je neema yake umemwagiwa, Tumeoshwa kwa damu ya kondoo? Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo? Wamwandama daima mkombozi Na kuoshwa na damu ya kondoo? Yako kwa msulubiwa makazi, Umeoshwa kwa damu ya kondoo? Atakapokuja Bwana –arusi Uwe safi kwa damu ya kondoo! Yafae kwenda mbinguni mavazi Yafuliwe kwa damu ya kondoo. Yatupwe yaliyo na takataka, Na uoshwe kwa damu ya kondoo. Huoni kijito chatiririka Na uoshwe kwa damu ya kondoo? ← Tenzi 79 | Tenzi Zote | Tenzi 81 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 79 – Msalaba Wa Aibu

Tenzi za Rohoni 79 – Msalaba Wa Aibu Tenzi Na. 79 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 79, “Msalaba Wa Aibu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Msalaba wa aibu, Ulinipa amani; Uliniondoa kifungoni, Nilimotesekea. Ee, Mwokozi wangu, Yesu Nitamwendea nani? Najiweka msalabani, Nikaoshwe damuni. Nakupenda Bwana Yesu, Kwa kunipenda kwako, Napendezwa nikutumikie Maisha yangu yote. Usifiwe Bwana Yesu, Kwa ulivyonifia, Aleluya, nakushukuru, Uliyenikomboa. Msalaba ulishinda Nguvu zake adui, Ili mimi nikombolewe, Niwe mwana wa Mungu. ← Tenzi 78 | Tenzi Zote | Tenzi 80 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 78 – Sioshwi Dhambi Zangu

Tenzi za Rohoni 78 – Sioshwi Dhambi Zangu Tenzi Na. 78 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 78, “Sioshwi Dhambi Zangu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hapendezewi Mungu, Bila damu yake Yesu. Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu. La kunisafi sina Ila damu yake Yesu. Wala udhuru tena, Ila damu yake Yesu. Sipati pataniswa, Bila damu yake Yesu. Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu. Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu. Wema wala amani, Bila damu yake Yesu. Yashinda ulimwengu, Hiyo damu yake Yesu. Na kutufikisha juu, Hiyo damu yake Yesu. Twaimba: Utukufu Una damu yake Yesu. Milele twaisifu, Hiyo damu yake Yesu. ← Tenzi 77 | Tenzi Zote | Tenzi 79 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 77 – Msalabani Pa Mwokozi

Tenzi za Rohoni 77 – Msalabani Pa Mwokozi Tenzi Na. 77 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 77, “Msalabani Pa Mwokozi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Msalabani pa mwokozi, Hapo niliomba upozi, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu. Chini ya mti msumbufu, Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu. Aliniokoa dhambini, Ikawa kunikaa ndani, Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu. Damu ya Yesu ya thamani, Huniokoa makosani, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu. Hicho kijito cha gharama, Leo jivike kwa kuzama, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu. ← Tenzi 76 | Tenzi Zote | Tenzi 78 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 76 – Njoni Enyi Wa Imani

Tenzi za Rohoni 76 – Njoni Enyi Wa Imani Tenzi Na. 76 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 76, “Njoni Enyi Wa Imani”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Njoni na furaha, enyi wa imani, Njoni Bethilehemu upesi ! Amezaliwa jumbe wa Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga, Amekuwa radhi kuzaliwa; Mungu wa kweli, wala si kiumbe; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu, Mbingu zote na zijae sifa; Sifuni Mungu aliye Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. Ewe Bwana mwema, twakubarikia, Yesu, utukufu uwe wako; Neno la Baba limekuwa mwili; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. ← Tenzi 75 | Tenzi Zote | Tenzi 77 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top