Skip to main content

Author name: contact@devinevisiontech.com

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 75 – Waimba, Sikizeni

Tenzi za Rohoni 75 – Waimba, Sikizeni Tenzi Na. 75 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 75, “Waimba, Sikizeni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni; Wimbo wa tamu sana Wa pendo zake Bwana, “Duniani salama, Kwa wakosa rehema.” Sisi sote na twimbe Nao wale wajumbe; Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni. Ndiye Bwana wa Mbingu, Tangu milele Mungu, Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali; Ametoka enzini Kuja ulimwenguni Mwokozi atufie, Ili tusipotee. Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni. Mtukufu wa amani Ametoka Mbinguni, Jua la haki, ndiye Atumulikiaye; Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi, Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya, Waimba sikizeni, Malaika Mbinguni. Njoo upesi, Bwana, Twakutamani sana; Kaa nasi, mwokozi Vita hatuviwezi; Vunja kichwa cha nyoka, Sura zako andika, Tufanane na wewe, Kwetu sifa upewe, Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni. ← Tenzi 74 | Tenzi Zote | Tenzi 76 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 74 – Wachunga Walipolinda

Tenzi za Rohoni 74 – Wachunga Walipolinda Tenzi Na. 74 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 74, “Wachunga Walipolinda”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Wachunga walipolinda Kucha nyama zao, Malaika mtukufu Alishuka kwao. Wakacha sana wachunga, Akawatuliza, “Nawaletea habari Ya kuwapendeza.” “Mji ule wa Daudi Leo amezawa Mwokozi ni Kristo Bwana, Ilivyoandikwa”. “Huyo mwana wa Mbinguni Ataonekana, Amelazwa kihorini Malazi hapana.” Alipokwisha yanena Malaika hao Waliimba wimbo huu Usio na mwisho: “Enzi ni yake Munju juu, Na nchi salama, Kwa watu nao radhi kuu, Sasa na daima.” ← Tenzi 73 | Tenzi Zote | Tenzi 75 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 73 – Yesu Zamani Bethrehemu

Tenzi za Rohoni 73 – Yesu Zamani Bethrehemu Tenzi Na. 73 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 73, “Yesu Zamani Bethrehemu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu zama Bethrehemu, Aliyezaliwa kwa aibu, Ndiye mwakozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi. Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi; Ndiye mwaokozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi. Yesu akafa msalabani, Kuniponya akalipa deni, Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi! Kunifia mimi! Kunifia mimi! Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi. Ni yeye huyo tangu asili; Na nilipotanga-tanga mbali Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi. Kuniita mimi; Kuniita mimi; Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi Yesu kristo atarudi tena, Hilo lanifurahisha sana. Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi. Kunijia mimi, kunijia mimi, Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi ← Tenzi 72 | Tenzi Zote | Tenzi 74 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 72 – Twendeni! Haraka!

Tenzi za Rohoni 72 – Twendeni! Haraka! Tenzi Na. 72 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 72, “Twendeni! Haraka!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza. Bwana alisema nendeni po pote Kawafundisheni mataifa yote. Pelekeni Injili kwa jina la Yesu. Upesi! Twendeni haraka! Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La upendo wa Mungu kwa watu wote; Aliyeupenda sana ulimwengu Akamtoa Yesu Mwana wake pekee Kaleta wokovu, tumtangazeni. Upesi! Twendeni haraka! Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La uzima kwa watu waliokufa. Mateka ya Shetani litafungua Litaponyesha na kuwapa amani. Twendeni upesi, tukawaokoe. Upesi! Twendeni haraka! ← Tenzi 71 | Tenzi Zote | Tenzi 73 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 71 – Mteteeni Yesu

Tenzi za Rohoni 71 – Mteteeni Yesu Tenzi Na. 71 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 71, “Mteteeni Yesu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mteteeni Yesu, Mlio askari; Inueni beramu, Mukae tayari, Kwenda nae vitani, Sisi hatuchoki Hata washindwe pia Yeye amiliki. Mteteeni Yesu, Vita ni vikali; Leo siku ya Bwana, Atashinda kweli, Waume twende naye, Adui ni wengi, Lakini kwake Bwana Tuna nguvu nyingi. Mteteeni Yesu, Wenye ushujaa; Nguvu zenu za mwili Hazitatufaa; Silaha ya injili Vaeni daima, Kesheni mkiomba, Sirudini nyuma. Mteteeni Yesu, Vita ni vikali, Wengi wamdharau, Hawamkubali, Ila atamiliki Tusitie shaka, Kuwa naye vitani Twashinda hakika. ← Tenzi 70 | Tenzi Zote | Tenzi 72 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 70 – Yesu Atuchunga

Tenzi za Rohoni 70 – Yesu Atuchunga Tenzi Na. 70 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 70, “Yesu Atuchunga”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Yesu atuchunga, Mchunga wetu, Naye atufuta Machozi yetu; Mkononi mwake Hatuna hofu, Daima twapata Kwake wokovu. Yesu atuchunga Tumemjua, Na sauti yake Twaitambua; Naye akituonya Ni kwa upole, Tu kondoo zake Hata milele. Yesu atuchunga; Aliwafia Kondoo wakubwa Na wana pia; Kwamba awajua, Kondoo zake, Hutiwa alama Ya damu yake. Yesu atuchunga; Mikono yake Imewaambata Kondoo zake; Hapati wadhuru Adui yule, Yesu awalinda. ← Tenzi 69 | Tenzi Zote | Tenzi 71 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 69 – Twendeni Askari

Tenzi za Rohoni 69 – Twendeni Askari Tenzi Na. 69 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 69, “Twendeni Askari”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Twendeni askari, watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, tumwandame juu. Ametangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini. Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu. Jeshi la Shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia, Kelele za shangwe zivume nchi; Ndugu inueni zenu sauti. Kweli kundi dogo, watu wa Mungu Sisi na mababa tu moja fungu. Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini moja, na moja dini. Haya mbele watu nasi njiani, Inueni myoyo, nanyi sifuni; Heshima na sifa ni ya Mfalme, Juu hata chini, sana zivume. ← Tenzi 68 | Tenzi Zote | Tenzi 70 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 68 – Mungu Msaada Wetu

Tenzi za Rohoni 68 – Mungu Msaada Wetu Tenzi Na. 68 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 68, “Mungu Msaada Wetu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Mungu msaada wetu Tangu myaka yote, Ndiwe tumaini letu La zamani zote. Kivuli cha kiti chako Ndiyo ngome yetu. Watosha mkono wako Ni ulinzi wetu. Kwanza havijakuwako Nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako Twakaa salama. Na myaka elfu ni kama Siku moja kwako; Utanilinda daima Tu wenyeji wako. Binadamu huondoka, Mwisho hana kitu; Kama ndoto hutoweka Ndivyo hali yetu. Ila wewe Mungu wetu Ndiwe wa kudumu; Ndiwe bora, ngome yetu Twakaa dawamu. ← Tenzi 67 | Tenzi Zote | Tenzi 69 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 67 – Bwana Uliyewaita

Tenzi za Rohoni 67 – Bwana Uliyewaita Tenzi Na. 67 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 67, “Bwana Uliyewaita”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Bwana uliyewaita Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa. Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? “Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana.” Nitume na mimi, Bwana Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia. Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini wewe waweza Kutufanya tayari. Neno lako tulijue, Tupe na roho yako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako. ← Tenzi 66 | Tenzi Zote | Tenzi 68 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Tenzi za Rohoni

Tenzi za Rohoni 66 – Po Pote Mashamba Yajaa

Tenzi za Rohoni 66 – Po Pote Mashamba Yajaa Tenzi Na. 66 Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 66, “Po Pote Mashamba Yajaa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza. Maneno ya Wimbo Po pote mashamba yajaa, Tele nafaka pevu, Po pote yang’aa meupe Bondeni na nyandani. Mwenye mavuno, wasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe. Wapeleke uchaoni, Waende na jotoni, Mpaka jua lishukapo Wakusanye ko kote. Watenda kazi wa Bwana, Mlete sasa mazao, Na jioni ingieni Kwake na furaha kuu. ← Tenzi 65 | Tenzi Zote | Tenzi 67 → Tazama Tenzi za Rohoni 1–164 Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top